GET /api/v0.1/hansard/entries/1407858/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1407858,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1407858/?format=api",
    "text_counter": 437,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mungatana",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 185,
        "legal_name": "Danson Buya Mungatana",
        "slug": "danson-mungatana"
    },
    "content": "hawapati lishe bora inayotakikana wakiwa wajawazito kwa sababu ya ukosefu wa pesa. Vituo vingi vya afya havina vifaa vya kutosha kusaidia kina mama kule Tana River wakati wa kujifungua. Nimefurahi kuona Mswada huu unaopendekeza kuwa mawaziri wa kaunti za Kenya nzima lazima wahakikishe kwamba watoto wetu na kina mama wajawazito wanatunzwa vilivyo. Najua kuwa Mswada huu ukipitishwa na Seneti, tutapata manufaa zaidi kwa kina mama na watoto wanaoletwa duniani. Wengi wetu tulinufaika sana na chanjo za bure za Serikali tulipokuwa watoto wadogo. Miaka hii imekuwa shida kupata chanjo katika hospitali zetu za kaunti---"
}