GET /api/v0.1/hansard/entries/1408675/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1408675,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1408675/?format=api",
"text_counter": 123,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante, Bw. Spika kwa kunipa fursa hii pia kutoa kauli yangu kwa Mswada wa ugawaji wa fedha kati ya serikali za kaunti na Serikali Kuu. Suala hili ni muhimu sana kwa sababu fedha hizi ndizo zinapeleka huduma katika kaunti zetu. Kwanza kabisa ni kuwa, wakati wa Kongamano la Ugatuzi mwaka jana kule Uasin-Gishu, Serikali ilitoa kauli kuwa itatoa zile huduma zote ambazo hazija gatuliwa. Lakini mpaka sasa hatujaona chochote kwa suala hilo. Hata hivyo, tukiangalia bajeti ya mwaka huu ambayo tunaizungumzia, inamaana kwamba suala la ugatuzi wa zile huduma zilizobakia litachukua muda zaidi kuliko vile ilivyo zungumziwa na Rais mwaka uliopita. Kwa sababu ya hiyo, ndio maana tunaona kwamba fedha zimebaki vile vile Kshs385 bilioni. Mwaka jana tulipitisha Kshs385 bilioni na wamependekeza kuongeza Ksh5 bilioni pekee ili zifike Kshs391 bilioni. Kila kaunti imeongeza gharama. Kuna miradi ambayo imekamilika na watu wakaajiriwa kazi. Huduma za kuendesha miradi kama zile zote zimoengezeka na hata bei za bidhaa pia zimeongezeka kwa sababu kumekuwa na ongezeko mara kwa mara la bei ya mafuta katika nchi yetu. Kwa hivyo, kuongeza Kshs4 bilioni ama Ksh5 bilioni kwa zile pesa ambazo zimetengwa kuja kwa kaunti ilikuwa ni makosa makubwa kwa Bunge la Kitaifa. Tulitoa mwongozo wakati tulipo jadiliana kuhusiana na kauli ama taarifa ya bajeti ‘ Budget Policy Statement’. Tulisema kwamba pesa ambazo zinatakikana kuja kwa kaunti ziongezwe ziwe Kshs415 bilioni. Nafikiri Bunge la Kitaifa lilipuuza kauli hiyo kwa sababu wangekuwa wameizingatia hawangeleta ile hesabu ya Kshs385 bilioni. Bw. Spika, kuna masuala mapya ambayo yameibuka. Kwa mfano, kodi ya nyumba ambayo imeletwa hivi juzi, ambapo kaunti na wafanyikazi wao wote wanastahili kulipa. Vile vile, kuna malipo mapya ya bima ya afya ambayo imeongezeka. Haya yote yameongeza gharama katika bajeti za kaunti zetu kuhusiana na malipo. Kwa hivyo, The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}