GET /api/v0.1/hansard/entries/1408676/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1408676,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1408676/?format=api",
    "text_counter": 124,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "pendekezo la kuongeza fedha hizi mpaka Kshs415 bilioni ni sawa kabisa. Tumeona pia kutoka ugatuzi uanze, zile pesa ambazo zinapelekwa katika kaunti zetu zinapungua kiasilimia. Mwaka jana ilikuwa asilimia 18 na mwaka huu imefika 15. Kila mwaka zina shuka. Hiyo haioneshi taswira nzuri ya ugatuzi katika nchi yetu. Bw. Spika, tungependa kuunga mkono pendekezo la kuongeza mpaka Kshs415 bilioni. Vile vile pia, tungependa kuona kwamba sheria ya ukaguzi ama sheria ya uhasibu wa fedha inabadilishwa, ili kuwe na uwezo wakati wameshindwa kupitisha zile hesabu za mwaka uliopita, iwe ni moja kwa moja fedha zinapita ili ziwe sambamba na zile pesa ambazo zinakusanywa katika nchi ya Kenya. Hatuwezi kutumia hesabu ya mwaka wa 2020, miaka minne iliyopita, kuamua pesa zitakazo kwenda kwenye kaunti zetu mwaka ujao. Ikiwa hesabu zetu za serikali za kaunti zimefika 2022/2023 ndizo zinazoangaliwa sasa, itakuwaje Serikali Kuu hesabu zake hazija angaliwa sawa sawa mpaka zikafikia mwako ambao tunaufuata. Kwa hivyo, hili suala la kucheleweshwa kwa kukaguliwa kwa hesabu za Serikali linachangia pakubwa pesa kidogo kuja katika kaunti zetu. Katiba inasema hatuwezi kuangalia kitu chochote isipokuwa hesabu za mwaka uliotangulia ama mwaka wa karibu kabisa ambazo zimeweza kuidhinishwa na Bunge la Kitaifa. Bw. Spika, hili ni suala la Kikatiba na nilazima tulivalie njuga kwa sababu tutaendelea kulalamika kila mwaka kuwa pesa zinazo kuja ni kidogo. Lakini tukiangalia kwa undani ni kwamba, tatizo liko katika Bunge la Kitaifa ambapo hawaangalii kwa haraka uhasibu wa fedha ambazo zimetumika katika serikali. Mwisho ni kwamba, mapato ya Serikali inaongezeka. Juzi wameanzisha malipo ya kila kitu kwa akaunti moja na ukilipa huwa kuna ile inayoitwa facilitation fee ya Ksh50. Kwa hivyo ikiwa kuna shughuli milioni moja kwa siku, inamaana wamekusanya Kshs50 milioni. Ikiwa watakusanya Kshs50 milioni kila siku kwa mwezi ni karibu Kshs1.5 bilioni. Pesa hii haiingii katika hesabu ya kaunti zetu. Ninafikiri pesa hii inatumika kwa Serikali pekee kwa sababu, fedha zile hazijawekwa katika orodha ya fedha ambazo tunastahili kupata kama kaunti. Bw. Spika, haya ni masuala ibuka ambayo ni lazima tuyaangalie kwa sababu haiwezekani fedha ziamuliwe na Hazina Kuu. Tulikuwa na pendekezo ya kuifanya hii Hazina Kuu kuwa huru kabisa, ili tuone kwamba wakiwa wanaangalia mahitaji ya kaunti wanaangalia lakini sio kwa sura ya Serikali kuu. Waangalie mahitaji ya kaunti kama taasisi huru. Hii itahakikisha kwamba kuna usawa katika kugawa raslimali katika nchi yetu ya Kenya. Asante kwa kunipa fursa hii."
}