GET /api/v0.1/hansard/entries/1408817/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1408817,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1408817/?format=api",
"text_counter": 265,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante, Bw. Spika wa Muda. Naunga mkono kamati zilizotuambia vile walivyofanya kazi kwa sababu wamefanya kazi nzuri. Tunajua katika ugatuzi, sisi Maseneta tunafaa tuendelee kufanya kazi ya kusaidia kaunti kupata pesa nyingi ndio kusitokee mambo kama yale yaliyotokea. Tunajua Kaunti nyingi hazina pesa za kutosha. Ndio maana wakati mwengine tunasema, “ni shilingi moja kwa mtu mmoja.” Hii ni kwa sababu kuna kaunti zingine zinazopata pesa lakini tukienda mashinani hakuna kazi imefanywa. Kuna kaunti zingine ziko na madeni makubwa. Wakati mwengine kunatokea vita kati ya governor na MCA . Kwa hivyo, naunga mkono ugatuzi uweze kutiliwa maanani. Unakuta mizigo mingi iko kwa magavana ilhali wako na kazi nyingi. Ndio maana unaona makosa mengine yamefanyika. Tumeona vile magavana waliochaguliwa katika hiki kipindi cha Serikali ya Kenya Kwanza pamoja na Azimio wanavyofanya kazi, hasa akina mama waliochaguliwa. Naunga Mkono kamati ya Sen. Osotsi. Hata hivyo, ni lazima tuangalie vile kaunti zilizo na madeni zitakavyopunguza madeni, ndio tuangalie vile tutasaidia kujenga zile kaunti zengine. Kama Seneti, tunahitaji pesa. Tunapaswa tuangalie namna ambayo Wabunge wa Bunge la Kitaifa watatupatia pesa ya kutosha. Asante. Naunga Mkono."
}