GET /api/v0.1/hansard/entries/1409487/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1409487,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1409487/?format=api",
    "text_counter": 270,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "(Mombasa County, ODM) Ahsante sana, Mhe. Spika. Nami pia napiga upondo majibu aliyotoa Mhe. Tongoyo. Mnazi unatumika vibaya hata kama ni kinywaji cha utamaduni. Wanaume wanatoka kwa Mnazi unaouzwa kuanzia saa kumi na mbili asubuhi. Hakuna mikakati ya kuweka wakati mwafaka. Wanaume wanalewa 24/7 kisha wanaenda kupiga na kuumiza wake wao. Mimi kama Mama kaunti ningepinga aina yoyote ya kilevya kama ingekuwa nguvu zangu. Nimekuwa nikiongea na Officer Commanding Police Division (OCPD) wa Jomvu mpaka jana. Anasema mpaka watoto wa shule wanatoka shuleni na kuingia kwenye mangwe yale kunywa Mnazi. Kwa hivyo, nakubaliana na ripoti aliyotoa Mhe. Tongoyo. Mnazi ni kilevya. Ni lazima kiwekewe mipaka. Kama ingewezekana, mimi pia ningesema kuwa Mnazi mwingi watoka Kilifi ukija Mombasa. Ningeweza ningeupinga ili usiingie katika kaunti yangu maanake watoto na watu wazima wanaharibika."
}