GET /api/v0.1/hansard/entries/1410102/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1410102,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1410102/?format=api",
    "text_counter": 239,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": " Asante sana, Mhe. Spika, kwa kunipatia hii fulsa ili niweze kutoa mchango wangu. Swala ambalo Mhe. Keynan alileta limekuwa donda sugu. Kila wakati vijana wanapotea, na hatujui vipi. Mombasa tumepoteza watoto wengi sana, na kila tukienda kufuatilia uchunguzi, hatupati njia mwafaka. Kawaida wakija kuwachukua, huwa wanajitambulisha kama maafisa wa Serikali. Lakini wakati ambapo tunaanza kufuatilia tujue hao watoto wako wapi, kila mmoja anakwepa. Kama wazazi na viongozi wa North Eastern na Mkoa wa Pwani, tuna wasiwasi sana vijana wetu wakipotezwa. Kwa hivyo, ningependa kumuelezea Mhe. pamoja na Waziri wakae na waangalie mambo haya ambayo yanatamausha sana. Ikiwa mtu amekosea, basi sisi tunaomba vyombo vya usalama wanapomshika wampeleke kortini afanye kesi. Ikiwa anayo hatia, basi afungwe, na sisi tutaridhika. Lakini, watoto kupotezwa hivi hivi, imetuuma sana na mimi ninaomba jambo hili lifuatiliwe kwa kina."
}