GET /api/v0.1/hansard/entries/1410471/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1410471,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1410471/?format=api",
"text_counter": 608,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, UDA",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": "Ninaeleza hivi, siku zote maji yanajua njia yake. Kwanza, ninawapa pole familia za Wakenya ambao wamepoteza wapendwa wao. Ni uchungu kuona kina mama wamezama ndani ya matope na watoto wamezama ndani ya maji. Watu wengi walipoteza maisha yao pale Tana River na Mai Mahiu. Hapa Athi River sikuona mafuriko ila kile kitu ambacho nimekiona pale ni watu walienda wakajenga sehemu za maji na maji siku zote yanajua mkondo wake. Maji yamekuja kuwatoa watu kwa nafasi yao. Hii nafasi ambayo watu wamejenga ni nafasi ya mkondo wa maji. Ndio maana sisi siku zote tunaambiwa kama Wakenya, hata kama unataka kununua sehemu ya kujenga jaribu uangalie historia ya sehemu hiyo. Wakenya wanaangamia kwa sababu wanadanganywa. Kwingine, idhibati za mashamba zinatoka kwa serikali ya kaunti na zingine national Government. Wanauzia watu sehemu ambayo ni kando ya maji. Nimeona sehemu ambapo maji yamejaa mpaka kwenye dirisha. Picha zimezungushwa zikionyesha watu wakisema ni mafuriko, lakini mimi leo ninasema yale si mafuriko bali ni maji imechukua sehemu yake, maji imekuja kuomba sehemu yake ilionyakuliwa na maji imeingia katika sehemu yake. Ni sehemu chache tu ambazo nimeziona ambapo barabara zetu hazikujengwa kwa uzuri au kwa design ya drainage. Ninamwambia Mhe. Murkomen achape kazi. Ninamwambia aangalie Kenya National Highways Authority (KeNHA), Kenya Urban Roads Authority (KURA) na hao ambao wanajenga mabarabara. Hata kule kwetu Nyali mabarabara hayapitiki kwa sababu wamejenga barabara lakini hawakuweka sehemu ya kupitisha maji. Kwa hivyo maji yanapata njia ya kwenda sehemu za nyumba. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor"
}