GET /api/v0.1/hansard/entries/1410472/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1410472,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1410472/?format=api",
"text_counter": 609,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, UDA",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": "Sheria ni msumeno, hukata mbele na nyuma. Na hata kama sisi tuko hapa kupigania Wakenya, lazima pia tuwambiane ukweli. Kuna wakati nimemuona Rais akiwaambia watu watoke sehemu za maji. Ukienda kujenga kwenye bonde ambapo maji yanapita na pia kando ya bahari, ile bahari itakuja kufurika na kubeba nyumba. Ile sehemu nimetaja haikuwa sehemu ya mtu aliyefunikiwa nyumba; ilikuwa sehemu ya maji na maji yamedai haki yake na maji yamerudi sehemu yake. Kwa hivyo, mimi ninawaomba Wakenya, mvua inapozidi kunyesha wakati huu, waondoke waende sehemu ambazo ni salama. Ondokeni muangalie sehemu ambazo mnaweza kukaa na familia zenu ikawa hamuwezi kuathirika na mambo haya. Maji yatazidi kuja kwa sababu nimeona mito nyingi iliyokuwa imekauka ikafanywa barabara, sasa maji yanarudi katika sehemu zile. Hakuna tena barabara, tunaziita mito Mhe. Naibu Spika. Kwa hivyo, mimi ninatoa rambirambi zangu na kumwambia yule ambaye ameshika shilingi bilioni sita katika ofisi ya Naibu Rais, atoe hizo pesa ziweze kuwasaidia wananchi ambao wanahangaika. Hizo ni pesa nyingi. Ningependa pia kumshukuru Naibu wa Rais. Nilimwona akizunguka kwa ndege akiangalia. Lakini hizo pesa ziko wapi? Azitoe ziweze kuwasaidia wananchi. Asante sana."
}