GET /api/v0.1/hansard/entries/1410514/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1410514,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1410514/?format=api",
"text_counter": 26,
"type": "speech",
"speaker_name": "Nyali, UDA",
"speaker_title": "Hon. Mohamed Ali",
"speaker": null,
"content": " Mhe. Spika, naomba kuwasilisha Hoja ifuatayo: KWAMBA, tukifahamu kuwa, Ibara ya 27(5) ya Katiba inaeleza kwamba hakutakuwepo na ubaguzi wa moja kwa moja au kwa njia isiyokuwa ya moja kwa moja dhidi ya mtu yeyote kwa msingi wowote, ikiwemo misingi ya dini; tukitambua kwamba baadhi ya taasisi za elimu za kidini kote nchini zinatekeleza wajibu muhimu katika utoaji wa elimu kwa wanafunzi wa imani mbalimbali za kidini; tukiwa na shauku kuwa kumekuwepo na ripoti za wanafunzi wa dini tofauti katika taasisi fulani za kielimu kukabiliwa na desturi za ubaguzi, ikiwemo kushurutishwa kuhudhuria ibada zisizolingana na dini zao; tukiwa na shauku zaidi kwamba pia kumekuwepo na matukio ya wanafunzi Waislamu kukatazwa kuvaa kulingana na mahitaji ya imani zao za kidini ambako kunawaathiri wanafunzi hao kwa njia hasi, ikiwemo kukwazika katika kaidi zao za kiimani, kuathirika kwa utendaji masomoni na mfadhaiko wa kisaikolojia; tukitambua kuwa ni muhimu kuunda mazingira jumuishi ya elimu na yenye heshima ambapo wanafunzi wote wanaweza kufanikiwa bila hofu ya chuki; pia tukitambua kwamba shule haziruhusiwi kuunda au kutekeleza kanuni zinazokiuka uhuru wa kuabudu, kama ilivyobainishwa katika Katiba; tukitambua ukweli kwamba hakuna sera ya kitaifa au mfumo wa kushughulikia na kuzua ubaguzi dhidi ya wanafunzi katika taasisi za kielimu za kidini; hivyo basi sasa, Bunge hili linaamua kwamba Serikali ya Kitaifa, kupitia kwa Wizara ya Elimu, iunde sera ambayo itaharamisha kwa njia bayana ubaguzi kwa msingi wa dini na kuhakikisha heshima kwa uanuwai wa dini kwa shule zote nchini na kutoa mfumo wa kufanya ukaguzi wa mara kwa mara na kuripoti matukio ili kushughulikia hali za ubaguzi na kuhakikisha ulinzi wa haki za wanafunzi."
}