GET /api/v0.1/hansard/entries/1411058/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1411058,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1411058/?format=api",
    "text_counter": 57,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Taita Taveta County, UDA",
    "speaker_title": "Hon. Haika Mizighi",
    "speaker": null,
    "content": "Nikirejelea mada yetu ya leo, ningependa kumpongeza dadangu Mhe. Ruweida kwa wazo hili zuri. Hili ni jambo ambalo lingefanyika kitambo sana. Kwa hivyo, ni vyema tulifanyie kazi sasa ili lianze kutekelezwa. Maafisa wa jeshi hufanya kazi kubwa sana katika nchi yetu na wanastahili heshima ipasavyo. Hatuwezi kusisitiza umuhimu wao zaidi. Tunapaswa kuwapa kipaumbele katika huduma mbali mbali. Kwa mfano, wanastahili kupewa kipaumbele wanapoabiri ndege na wanapoendea huduma za benki. Tumetembea nchini mbali mbali Ulaya na hiyo ndiyo hali ilivyo. Kwa mfano, kule Marekani, wanajeshi hupewa discount maalum. Hapa Kenya, bado hatutambui maafisa wetu."
}