GET /api/v0.1/hansard/entries/1411145/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1411145,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1411145/?format=api",
"text_counter": 144,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kisauni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Rashid Bedzimba",
"speaker": {
"id": 13383,
"legal_name": "Ali Menza Mbogo",
"slug": "ali-menza-mbogo"
},
"content": "Hoja hii inasema maafisa wa jeshi wakipanda ndege, wapatiwe kipaumbele. Ni kweli mataifa mengi sana nimeenda, hata Uturuki, wanapewa kipaumbele. Wakiwa ndani ya ndege ya abiria ama ndege ya aina yeyote, chochote cha usalama kikitokea, wanaingia kazini. Hawawezi kusema wako katika likizo . Kwa hivyo, ni vyema wapewe nafasi hiyo, ingawa si wanajeshi wote wanapanda ndege. Kuna wengine wanapanda matatu. Wengine wanatembea. Tutafute njia ya kuwaheshimu na sio tu wale wanaopanda ndege. Hata wale wanaotembea wapatiwe kipaumbele katika ofisi zote za Serikali zinazotoa huduma. Chochote kikitokea ni lazima kitangazwe na wanajeshi wote waambiwe warudi kambini saa hiyo na kuelezwa kilichojiri. Ikiwa ameenda Huduma Centre ama ofisi ya Serikali, apatiwe kipaumbele na familia yake na atoke mahali pale haraka."
}