GET /api/v0.1/hansard/entries/1411162/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1411162,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1411162/?format=api",
    "text_counter": 161,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kwale County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Fatuma Masito",
    "speaker": null,
    "content": "Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii ili nitoe pole zangu kwa familia za wanajeshi wetu waliofariki hivi majuzi katika ule mkasa wa ndege. Nasema pole sana. Kama Waislamu, tunaamini kuwa kuna mauti na kila mtu aliyezaliwa lazima siku moja atafikiwa na mauti. Hakuna kitakachobaki katika dunia hii. Lakini mauti yakitokea kwa njia ya kutatanisha, si vibaya uchunguzi ukifanywa ili ijulikane kiini cha kifo kile. Hoja hii iliyo mbele ya Bunge hili ni ya kuwasaidia ndugu zetu wanajeshi walio nje na ndani ya taifa hili, na kuwapongeza kwa kazi nzuri sana wanayoifanya. Lakini naona Serikali yetu bado haijawatambua. Wanajeshi wanafanya kazi ngumu ya kujitolea ambayo hata mimi na wewe tukipewa, nina uhakika tutaiona ikiwa ngumu. Wanakaaa nje siku nyingi au masaa mengi mbali na familia zao. Ingekuwa kazi ngumu kwangu kukaa mbali na familia yangu ili kuhudumia taifa. Ningependa Serikali iwaangalie wanajeshi ili wapate heshima mahali popote wanapotembea na wapate makaazi mazuri. Waheshimike wanaposafiri na wanakoishi. Utapata hata sehemu zao za makaazi na malazi ni duni sana. Ingekuwa vyema ikiwa katika hali ya kuwaheshimu kwa kazi ngumu wanayofanya, wapewe priority kila mahali wanapoingia. Hawa The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor"
}