GET /api/v0.1/hansard/entries/1411404/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1411404,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1411404/?format=api",
    "text_counter": 152,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Likoni, ODM",
    "speaker_title": "Mhe. Mishi Mboko",
    "speaker": null,
    "content": " Asante sana, Mhe. Spika. Nimesimama kuunga mkono Mswada huu wa mambo ya Tume ya Uchaguzi. Mswada unasema kwamba kutakuwa na upanuzi wa jopo la uteuzi wa Tume ya Uchaguzi kutoka watu saba mpaka watu tisa. Hii italeta watu zaidi ambao wana taaluma mbalimbali kushirikiana kuhusu mambo ya uchaguzi katika taifa letu la Kenya. Pia itawezesha kutoa zile tofauti ambazo zimekuwa hapo mbele ama yale malalamiko ambayo yamekuwa, haswa tukizingatia vile ile jopo liliundwa. Baada ya watu kushikana pamoja na kuzungumza ili kupata uwiano, ni vyema tuwe na hao watu tisa katika jopo ili tupate taaluma tofauti tofauti na tuwe na uwazi zaidi. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor"
}