GET /api/v0.1/hansard/entries/1411670/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1411670,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1411670/?format=api",
    "text_counter": 62,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Nakuru Town East, UDA",
    "speaker_title": "Hon. David Gikaria",
    "speaker": null,
    "content": " Asante sana, Mhe. Spika, kwa kunipatia nafasi hii. Natoa rambirambi zangu kwa familia za wanajeshi wetu ambao walipata ajali na kufariki walipokuwa kwenye kazi zao. Nichukue nafasi hii kutoa rambirambi kwa familia ya kijana mmoja kutoka Nakuru County, mahali baba yake anaishi, na amekuwa akitumikia kwa muda mrefu. Kijana huyu ni Captain Hillary Litali na alikuwa anaishi mtaa wa Shabab ulio sehemu ya Nakuru West. Mhe. Spika, alikuwa kijana mdogo sana wa miaka 29 na alikuwa karibu kupatiwa cheo cha Major kwa kazi nzuri aliyokuwa akifanya. Alikuwa kijana wa kwanza katika familia changa. Cha muhimu ni kuweka tahadhari kwa watu wa social media . Hii ni kwa sababu wanatangaza vifo vya watu kabla familia ifikiwe kupitia njia rasmi. Wanafaa wakomeshwe kupitia sheria zetu ambazo tulipitisha."
}