GET /api/v0.1/hansard/entries/1411679/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1411679,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1411679/?format=api",
"text_counter": 71,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu East, JP",
"speaker_title": "Hon. Ruweida Mohamed",
"speaker": {
"id": 2100,
"legal_name": "Shariff Athman Ali",
"slug": "shariff-athman-ali"
},
"content": "Mhe. Spika, pia nachukua nafasi hii kutoa rambirambi kwa familia za maafisa wote wa KDF waliofariki wakifanya kazi ya kuchunga nchi yetu. Sisi wana Lamu Mashariki tunatumia KDF tunapopatwa na jambo. Hili ndilo eneo Bunge pekee ambalo walimu hupelekwa shule kama wamebebwa na KDF. Shule zote ambazo ziko Boni Forest lazima watu wabebwe na KDF."
}