GET /api/v0.1/hansard/entries/1411834/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1411834,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1411834/?format=api",
"text_counter": 226,
"type": "speech",
"speaker_name": "Likoni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Mishi Mboko",
"speaker": null,
"content": "walikuwa ni walengwa ama ni wale wale ambao walipata kupitia njia za kisiasa zisizo sawa? Hii itatusaidia kutathmini hali. Vile vile, Mhe. Owen amekizungumzia Kifungu 15(3) na kusema lazima kifutwe. Hii ni kwa sababu kikiwa hapo, kitakuwa pingamizi katika kutekeleza shabaha za Tume ya Ardhi. Wakenya walizungumzia kuwepo kwa Tume ya Ardhi kwa sababu Wizara ilikuwa hapo kwa miaka mingi sana na haikuweza kutathmini, haswa kuangalia zile dhuluma za kihistoria za mambo ya ardhi. Kwa mfano, Serikali iliangalia ile ardhi ya Mazrui iliyoko sehemu za Kilifi na ikasema kuwa itapeana pesa kwa wahusika ili kusaidia maskwota walio pale wapewe ardhi. Iwapo Tume ya Ardhi itasitishwa kufanya kazi yake, mambo kama haya ambayo yamefanyika yatakuwa ni shida. Itabidi tena turudi mwanzo ili tuone jinsi ya kutatua tatizo hili nyeti. Ukiangalia sehemu ya Bonde la Ufa, kuna matatizo mengi ya ardhi kupitia dhuluma za kihistoria. Pia Pwani, matatizo kama hayo ni mengi. Katika sehemu za kati nchini, vile vile tumeona matatizo hayo. Kwa jumla, Kenya nzima inayo haya matatizo."
}