GET /api/v0.1/hansard/entries/1411886/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1411886,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1411886/?format=api",
"text_counter": 278,
"type": "speech",
"speaker_name": "Wundanyi, WDM",
"speaker_title": "Hon. Danson Mwashako",
"speaker": null,
"content": " Asante Mhe. Naibu Spika. Masuala ya ardhi ni masuala nyeti ambayo Bunge la Taifa likipata nafasi ya kuyajadili, ni muhimu sana tuwe na watu wengi ambao wanazungumzia masuala haya. Kwanza nampongeza Mhe. Owen Baya ambaye ameleta Mswada huu kubadilisha kipengele cha 14 cha Sheria ya Tume ya Kitaifa ya Ardhi, kinachosema kwamba tume ilikuwa na miaka mitano pekee kuangazia dhulma za kihistoria kuhusiana na mashamba. Mhe. Naibu Spika wa Muda, masuala ya mashamba ni mazito. Wenzangu, ikiwemo Mbunge wa Malindi, wamechangia Mswada huu na ni vizuri sana umeletwa na Mbunge wa Pwani. Hii ni kwa sababu sisi tumepata shida zaidi kuliko wenzetu wa sehemu zingine za Kenya. Dhulma za mashamba za kihistoria zimekuwa donda sugu kwetu. Nikikupatia tu mfano mdogo, kando na mashamba ambayo yalichukuliwa na wazungu ama mabwenyenye, kuna mashamba ambayo yalichukuliwa hata na idara za Serikali. Kama mfano, Shirika la Wanyama Pori (KWS). Kule Taita Taveta, KWS ilichukua asilimia 62 ya shamba la Taita Taveta. Idara ya Magereza pia ilichukua mashamba mengi sana. Si Taita Taveta peke yake lakini ninajua ndani ya nchi yetu imechukua mashamba makubwa. Ukiangalia sana, mashamba yale yaliyochukuliwa na KWS na Idara ya Magereza na mashirika mengine, yamebaki hata bila kutumika ilhali wananchi wanakosa sehemu za kufanyia maendeleo. Tunavyojua ni kwamba shamba ndio kiungo muhimu sana katika uzalishaji wa mapato nchini. Kwa hivyo, kuendelea kuipatia fursa Tume ya Mashamba nchini ili kuangazia changamoto zilizoletwa na mashamba yaliyochukuliwa kinyume cha sheria na dhulma ambazo zimekuja kupitia mambo haya ya mashamba, ni jambo la kuungwa mkono. Kwa hivyo, mimi naunga mkono sheria hii. Kuna mabwenyenye ambao walichukua mashamba lakini hata leo, hawayafanyii chochote na nchi yetu tumekuwa tukitafuta sana jinsi ya kuongeza mapato ya nchi. Kando na kuongeza muda wa kuchunguza mambo haya, Bunge hili liweze kuangazia sana jambo la ushuru wa mashamba unaojulikana kwa Kizungu kama"
}