GET /api/v0.1/hansard/entries/1411889/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1411889,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1411889/?format=api",
"text_counter": 281,
"type": "speech",
"speaker_name": "Wundanyi, WDM",
"speaker_title": "Hon. Danson Mwashako",
"speaker": null,
"content": "Hata tunapoiongezea muda Tume ya Ardhi ni lazima pia wao wawajibike kwa sababu kuchanganyikiwa kwingi kwenye mambo ya mashamba nchini kumesababishwa na hii tume ya NLC. Mara nyinyi tukiwaita waje wawafafanulie wananchi mambo ya mashamba yaliyochukuliwa kutoka kwao ilhali wanasema kuwa wako na hati miliki, watu wa NLC huwa wanachelewa. Hawataki kuja kukutana na wananchi ili wawaelezee kinaga ubaga kuhusu msimamo wa sheria kuhusu shamba lile. Kwa hivyo, tunapowaongezea muda wa kuchunguza mambo haya, ni lazima pia wawajibike katika utendakazi wao. Nimeandika barua kutoka kwa ofisi yangu na ninawatarajia waje kuwaona wananchi kule Taita Taveta ili wawaeleze haswa msimamo wa serikali na tume ile kuhusu shamba la Taita Estate. Ikiwa wananchi watalazimika kuwekeza fedha ili wanunue shamba lile, wawe na uhakika kuwa wanafanya jambo ambalo liko sawa kisheria. Kama kuna tatizo la umiliki wa shamba lile, basi NLC ije na iseme wazi kuwa kuna shida. Lakini wakiwacha watu in abeyance na hatujui ukweli uko wapi, basi wanatuchanganya. Tulipotangaza rasmi Katiba mpya mwaka wa 2010, muda wa lease wa mashamba wa miaka 999 ulipunguzwa mpaka miaka 99 lakini bado kuna mashamba mengi ambayo mpaka leo hatuna uhakika kuhusu umiliki wao kwa sababu wenyewe wanauza shamba hizo. Kwa sababu wale wanaouziwa shamba hizo hawafuatilii sheria sana, wananunua shamba ambazo miaka ya lease iliyobaki ni kidogo. Kwa hivyo, hii NLC ina nafasi kubwa ya kutatua shida za shamba nchini. Ninaunga mkono Mswada huu kwa sababu ninajua tumepata shida, hasa watu wangu. Watu wa Pwani na sehemu nyingine nchini Kenya wamepata shida. Kuna hatimiliki zilizotolewa na Wizara ya Ardhi kisha, NLC wakasema kuwa hatimiliki hizo sio sawa. Ni lazima Wizara ya Ardhi na NLC wajifunze kufanya kazi pamoja ili wasiwachanganye wananchi. Tuna title deeds ambazo NLC waliandika barua na kusema kuwa ni fake, lakini tukienda kwa Wizara, wanatuambia title deed s ziko sawa. Ni lazima Serikali ya Kenya Kwanza itoe mwelekeo. Mheshimiwa Owen yuko hapa. Kuna titles ambazo zimekataliwa na NLC, na kuna zile ambazo Wizara imesema ziko sawa. For us to solve maswala ya shamba, ni lazima Kenya Kwanza comes up with a clear land policy ya kusema kuwa questionable titles zirudishwe, na watoe msimamo kamili wa Serikali ili wananchi waelewe maswala haya yataenda vipi. Hivi karibuni, nyumba za watu zilibomolewa kule Voi. Watu wa Msambweni walivunjiwa nyumba zao kwa sababu mwenye ardhi hana hatimiliki. Wananchi walijulishwa kuwa Serikali inafuatilia maswala hayo. Ilipofika siku ya kubomoa nyumba, Kamishna wa Kaunti na wakubwa wa polisi walikuja na bunduki na kusimamia ubomoaji huo. Ninataka kukashifu swala hilo ingawa lilipita. Korti inapopeana ruhusa ya kubomoa nyumba za watu, Kamishna Wa Kaunti, vyombo vya Serikali na Wizara husika hawana ruhusa ya kuja na bunduki na kutishia wananchi wanapotoa vitu vyao pole pole. Wanapaswa kuketi na mwenye shamba na kuzungumza naye. Maswala haya ni lazima …."
}