GET /api/v0.1/hansard/entries/1411891/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1411891,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1411891/?format=api",
    "text_counter": 283,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Wundanyi, WDM",
    "speaker_title": "Hon. Danson Mwashako",
    "speaker": null,
    "content": "Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda. Ningekupa kura yangu kama ungekuwa unagombea kiti cha urais. Mhe. Spika wa Muda, tumepoteza watu kule Msambweni. Nilikuwa pale siku ya ubomoaji wa nyumba. Waliosimamia ubomoaji ule ni polisi waliokuja na wakubwa wa polisi na Kamishna wa Kaunti. Watu walikuwa wanasumbuka, wanalalamika, na kupata shida lakini wale ambao walipewa nafasi ya kuweka usalama walikuwa wameketi pale na kuruhusu ubomoaji wa nyumba za watu. Ninataka kukemea visa hivyo. Rais William Ruto alisema kuwa akiwa mamlakani, nyumba za watu hazitabomolewa. Ninataka Mhe. Owen amkumbushe Rais kuwa alisema nyumba za watu hazitabomolewa tena. Tunaomba kuwa jambo lililotendeka pale Msambweni, Voi lisiwahi kutendeka kwingine. Watu wa Voi bado wana wasiwasi kuwa The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor"
}