GET /api/v0.1/hansard/entries/1411905/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1411905,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1411905/?format=api",
"text_counter": 297,
"type": "speech",
"speaker_name": "Msambweni, UDA",
"speaker_title": "Hon. Feisal Bader",
"speaker": null,
"content": " Asante sana kwa kunipa nafasi hii niongeze sauti yangu kwenye huu Mswada ulioletwa na Mheshimiwa Owen Baya. Vile vile, nampongeza Mheshimiwa Owen Baya kwa kuuzingatia na kuuleta hapa ili Tume ya Ardhi iongezwe muda wa kufanya kazi waliyopatiwa na Katiba ya Kenya. Suala la ardhi ni muhimu sana na nyeti. Tume ya Ardhi iliundwa kuangazia mambo mengi. Mojawapo ni kuangalia dhuluma za kihistoria. Nikisema dhuluma za kihistoria, sisi Wapwani tumedhulumiwa sana kuhusu masuala ya ardhi yetu. Nazungumza hapa nikiwakilisha Eneo Bunge la Msambweni. Mpaka leo, sisi ni Maskwota katika kijiji nilichozaliwa. Uskwota ule umesababishwa na dhuluma kwa sababu umiliki wa ardhi yote – Zaidi ya ekari elfu nne – umeshikiliwa na mabwenyenye wawili peke yake. Wananchi wa pale, zaidi ya familia elfu tano, tunakaa katika ekari kumi na tatu pekee. Kwa hivyo, Mswada huu utaipa nguvu Tume ya Ardhi iendelee kupokea malalamishi na kuyatatua ili Wakenya na Wapwani waweze kumiliki ardhi zao. Tuko na matatizo mengi ya ardhi. Mpaka sasa, hatuwezi kufanya maendeleo katika sehemu zetu. Nina wadi moja katika eneo bunge langu iitwayo Ukunda ambako kuna changamoto nyingi sana. Mpaka sasa hatuwezi kuweka mradi wowote wa kimaendeleo katika wadi hii. Kwa hivyo, naomba Wajumbe wenzangu katika Bunge hili waunge Mswada huu mkono ili upitishwe na Wakenya wapate hatimiliki na kumiliki ardhi zao kihalali."
}