GET /api/v0.1/hansard/entries/1412187/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1412187,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1412187/?format=api",
    "text_counter": 171,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Likoni, ODM",
    "speaker_title": "Mhe. Mishi Mboko",
    "speaker": null,
    "content": "mara nyingi tunawaumiza watumiaji na waekezaji ambao wanakuja kwenye kaunti zetu kuboresha uchumi. Mswada huu umezungumzia wakati kaunti inataka kubadilisha malipo ya leseni lazima ifanye mkutano na washikadau, ile tunaita kwa Kiingereza public participation. Wazungumzie swala lile kwamba wamebadilisha yale malipo. Hivi sasa unapata katika kaunti nyingi, wanaamka tu na wanasema pengine kwamba kuegeza gari limepandishwa, na mtalipa pesa hizi. Ama ile pesa ya cess imepandishwa, na mtalipa pesa hizi, pasi na kuwahusisha wale washikadau. Vilevile, Mswada huu umezungumzia kwamba yale malipo yatakayowekwa hayatakuwa ya kuumiza yule mtumiaji ama muwekezaji. Yatamwezesha yule mwekezaji ama mtumiaji wa bidhaa. Iwapo mtu anataka kupata zaidi ya leseni moja, Mswada huu unaonyesha taratibu ambazo zitafuatwa ndio asiwe na ugumu wa kuweka yale maombi ya leseni. Kwa hivyo, kutakuwa na taratibu za usawa, pasi na kuumiza watumiaji. Pia, Mswada unasema huduma na bidhaa zinapaswa ziwe bora. Sio eti kutakuwa na huduma tu ambayo si bora, ama kutakuwa na bidhaa ambazo si bora. Lazima ziwe ni bidhaa na huduma bora. Vilevile kutakuwa na kanuni ama alama ya siri, ile kwa Kiingereza tunaita code . Kutakuwa na alama za siri tofauti katika kila leseni ambayo mtu atakua ameomba. Tukiwa na moja tu, hapo huwa tunakuwa na mchanganyiko na tunaleta shida kwa wale watumiaji ama waekezaji. Tutakuwa na hizo alama za siri ama kanuni tofauti katika kila kaunti. Haiwezi kuwa kaunti ya Kilifi na Nakuru itakuwa na hiyo alama moja. Tukifanya hivyo, tunaleta tofauti ama sintofahamu kwa wale watumiaji wakati wameweka maombi ya kupata leseni zile. Mswada huu umerahisisha ama kuweka mambo wazi na umeleta uwajibikaji katika kupata leseni. Utumiaji unaeleza malipo ya leseni yatakavyolipwa yatakuwa ni kwa njia gani. Tumekuwa na shida sana. Wananchi wengi wanalia. Unapata tu mambo yanaongezwa kila uchao. Tukiangalia hali yetu ya kiuchumi vile ilivyo, japokuwa sasa hivi tunaona mambo pengine huenda yakabadilika yakawa mazuri, Wakenya wengi bado wanapata shida sana kwa sababu hakuna sheria mwafaka kama hizi. Tukiwa na sheria ya kitaifa ambayo itakuwa imesimamia kaunti zote, basi hakuna gavana ama kaunti ambayo itaenda kinyume kwa sababu sheria ni msumeno na inakata mbele na nyuma. Lazima ifuatwe. Mbali na yale mambo mengi ambayo yatafanya, pia katika mambo yetu ya mazingira, ile tunaita kwa Kiingereza environmental protection, sheria hii itachunga mazingira. Mswada huu pia umezungumzia zile taratibu ama njia zitawekwa ziwe ni nyepesi na wananchi apate maelezo. Tunasema access to information ; awe anaweza kupata maelezo pasi na kuwa na vizuizi. Katika jambo hili, kuna mambo mengi sana ya ufisadi. Unapata mtu anaambiwa akitaka leseni ama fomu lazima kwanza achotee mtu. Tunataka Mswada huu uwe na wepesi wa kupata maelezo na taratibu zinazohusika katika mambo ya kupata leseni. Nimefurahishwa sana na jambo hili kwa sababu litahusisha washikadau. Kwa hivyo, hakutakuwa na pahali mshikadau atalalamika na aseme hakujua au hakuhusishwa mambo yanapoenda kwa njia ambayo haikuwa imepangwa. Naibu Spika, ninakushukuru sana kwa sababu unaenda kwa mkutano mwingine muhimu. Niwaambie Wabunge wenzangu, kesho Rais atakuwa katika maeneo ya Bunge Tower kutufungulia jumba lile kirasmi. Nyote mnaalikwa. Poleni, haikuwa mada hiyo, lakini ninawaalika. Ahsante."
}