GET /api/v0.1/hansard/entries/1412429/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1412429,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1412429/?format=api",
    "text_counter": 155,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Endebess, UDA",
    "speaker_title": "Hon. (Dr) Robert Pukose",
    "speaker": null,
    "content": " Ninakushukuru, Mheshimiwa Spika wa Muda. Ninaiunga mkono Hoja hii ambayo imeletwa na Mhe. Dorothy Ikiara kuwa Serikali iwape marupurupu wale wanaowahudumia walemavu ili wanapowachunga, wawe na kitu kinachowasaidia kuwahudumia katika hali nzuri. Hili ni jambo zuri. Ningependa kumuomba Mhe. Dorothy abadilishe Hoja hii ili iwe sheria na ahakikishe kuwa the Ministry of Labour and Social Protection iunde Regulations ili tusipitishe tu Hoja hii ilhali wale wanaotoa huduma hawapati marupurupu yao. Tutakuunga mkono wakati huo ili tuhakikishe kuwa Hoja hii iwe sheria ili wanaohudumia walemavu wapate marupurupu kutoka kwa Serikali."
}