GET /api/v0.1/hansard/entries/1412518/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1412518,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1412518/?format=api",
    "text_counter": 244,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Jomvu, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Bady Twalib",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante sana Mhe. Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii pia nichangie huu mjadala muhimu. Mjadala huu ni muhimu sana kwa sababu ni jana tu tukiwa na Mhe. Bedzimba wa Kisauni, tulizungumza maneno kama haya tukiwa katika kikao kimoja ambacho tulikuwa tumealikwa. Mhe. Spika wa Muda, mimi ni mwanakamati wa Kamati ya Barabara na Uchukuzi. Kama alivyosema Mwenyekiti wangu, saa moja lililopita, tulikuwa katika KICC ambako Mhe. Rais alizindua mambo ya usalama barabarani. Hivi leo yale ambayo yaljiri huko ni yale ambayo wanenaji wezangu wameyasema. Hatuwezi kumbwagia Waziri Murkomen matatizo makubwa. Alizungumza pale na kusema kuwa katika survey iliyoangaliwa vizuri sana, tatizo kubwa sana kuhusu ajali na matatizo ya barabarani yanasababishwa na madereva ambao wanafanya shughuli hizo. Hawa ni madereva wa mabasi, matatu au pikipiki. Mhe. Spika wa Muda Rais alisema kuwa kando na mikakati yote, idadi ya ajali za barabarani zimepanda. Alimpa jukumu Mhe. Waziri Murkomen kwa kusema kuwa mkutano kama huu utafanyika mwaka ujao na anataka ripoti kuthibitisha kuwa ajali za barabarani zimepungua."
}