GET /api/v0.1/hansard/entries/1412519/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1412519,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1412519/?format=api",
    "text_counter": 245,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Jomvu, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Bady Twalib",
    "speaker": null,
    "content": "Mhe. Spika wa Muda, ninakubaliana na yale yamezungumzwa. Mhe. Murkomen alisema mtu wa boda boda anaenda kwa uwanja wa mpira na anazunguka raundi mbili ama tatu, anafunzwa bila leseni na kesho anaingia barabarani anakuwa dereva wa pikipiki. The NTSA imeambiwa leo iache mvutano na polisi. Rais ametoa maelekezo leo. Amesema Mkurugenzi Mkuu wa NTSA, Bwana Njao, na Mkuu wa Polisi, Bwana Koome, wasing’ang’anie kusema hii ni mamlaka ya nani. Afisa wa NTSA na polisi wanajukumu la kulinda wananchi wa Kenya katika barabara zetu. Unaona mtu ametoka na familia yake, na kwa sababu ya uzembe wa dereva, anapata ajali na familia nzima inapoteza maisha. Nikiwa Mwanachama wa Kamati ya Kiidara ya Uchukuzi, Ujenzi wa Miradi ya Umma na Makazi, ninasema ule uzinduzi tumefanya leo na Rais utaonyesha ikiwa ni safety belt tunatakikana tufunge, tutaweka system ambayo usipofunga, inaonekana mpaka ofisi kuu ya NTSA. Ikiwa ni speed governor itaonekana, na kutawekwa cameras ambazo wameonyesha leo. Ikiwa ni uzembe wa dereva, utaonekana ili ujulikane. Kama Kamati, tunashukuru tukiangalia kule kwetu Mombasa, hasa katika Eneo Bunge langu la Jomvu. Zamani ajali zilikuwa nyingi sana, kwa sababu ya barabara mbovu. Lakini, ninashukuru leo kwa sababu tuna barabara kuu ambazo zimetengenezwa."
}