GET /api/v0.1/hansard/entries/1412558/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1412558,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1412558/?format=api",
"text_counter": 284,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kisauni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Rashid Bedzimba",
"speaker": {
"id": 13383,
"legal_name": "Ali Menza Mbogo",
"slug": "ali-menza-mbogo"
},
"content": " Asante sana, Mhe. Spika wa Muda kwa kunipa fursa ya kuchangia suala hili la ajali barabarani ambalo limeleta hasara kubwa katika taifa letu. Ni huzuni kubwa jinsi tanavyopoteza maisha katika barabara zetu. Pia, kuna kubadilishwa kwa hali ya kimaumbile ya watu wetu; mtu anatoka nyumbani akiwa mzima na anaporudi baada ya wiki moja ni mlemavu. Hiki ni kitu cha kusikitisha sana katika barabara zetu. Mhe. Bady ambaye ni mwanakamati wa Kamati ya Uchukuzi, amezungumza wazi wazi juu ya mambo ambayo yanafaa kurekebishwa. Mimi nitazingatia Wizara ya Barabara. Wizara hii inahitajika kuwekeza ili ipunguze ajali. Ukienda nchi za Ulaya na nchi jirani kama vile Rwanda na Tanzania, idadi ya visa vya ajali imerudi chini. Hapa kwetu, shida ni kuwa tuna ajali nyingi. Watu wakitaka kutoka wasafiri asubuhi kama familia, wataomba sana maombi ya kufika salama, kuenda kaburini, na kuamkia huko kwa sababu hawana uhakika wa kufika. Wanapokuwa barabarani, wale waliowaacha nyumbani huwa na wasiwasi na huwapigia simu kuhakikisha kuwa wamefika salama ndio washukuru. Hii ni kwa sababu barabara zetu zina matatizo. Hiii Wizara ihakikishe imesoma sehemu zile zingine. Kuna barabara zimetengenezwa ndogo kwa upana hadi kupishana ni shida. Madereva wa Kenya ni wazuri sana wakienda nchi za Ulaya kwa sababu barabara ni pana na wanaweza kupishana na madereva wengine. Ajali nyingi hapa ni gari kwa gari kwa sababu mmoja anataka kupishwa na mwingine amefika. Ni kwa sababu barabara zimefinyika sana. Vile vile, Wizara lazima iweke ishara kwenye barabara ya kuonyesha kona mbaya au mahali pana teleza kukinyesha. Hakuna ishara hapa. Ni wewe uende tu. Hata ishara ya kizuizi mwendo hakuna. Utaenda upande ghafla kisha ujipate msituni ama uwagonge wanaouza mboga kando ya barabara. Lingine ni ushirikiano baina ya washika dau wote wa masuala ya barabara. Ikiwa mabasi yanasababisha ajali, lazima Wizara iwaite washika dau kuzungumza nao kujua mahali shida iko. Ikiwa madereva wanafanyishwa kazi ya ziada, mtawaeleza utaratibu unaofaa. Hapa kwetu hakuna kuita washika dau. Mtu anakaa ofisini na kuamua kuanzia kesho huyu dereva anafaa kushikwa. Hiyo haiwezi saidia taifa. Lazima watu wakae chini wajadiliane. Kuna polisi wazuri na kuna wale wanapenda pesa. Mkijua yule ambaye anapenda pesa, mwacheni akalinde benki halafu mlete wengine wakulinda barabara. Anayependa pesa awekwe karibu na benki ahesabu na kunusa harufu ya pesa na maafisa wazuri wawekwe barabarani kusimamisha magari na kushtaki madereva kwa haki, na sio kwa sababu hawajapatiwa Ksh200. Ni sisi wenyewe kama serikali tupange mambo, siyo masuala ya madereva. Ikiwa dereva amefanya ajali mara ya kwanza na kushtakiwa, akifanya mara ya pili basi ako na doa. Leseni yake ichukuliwe. Sio kuamka na kusema madereva watarudi mafunzo. Sio wote ambao wako na matatizo. Ningependa kuendelea zaidi, lakini Mhe. Zamzam ana maneno mazuri. Akipewa nafasi kwa muda wangu, kutakuwa kuzuri. Asante sana, Mhe. Spika wa Muda."
}