GET /api/v0.1/hansard/entries/1412612/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1412612,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1412612/?format=api",
    "text_counter": 38,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante sana, Mhe. Spika. Ningependa kuchukua fursa hii kukushukuru kwa kazi nzuri ambayo umefanya. Si vizuri kuwa kila kitu kinapingwa kwa sababu kuna mambo mazuri mnayoyafanya, na ni ya kupigiwa upeto. Lile jumba limekaa miaka mingi, lakini wakati wako umehakikisha kuwa limekamilika. Mimi nimetembea pale na mambo yako shwari kabisa. Kwa hivyo, usisikilize fitina za huku na kule. Kuwa ngangari. Sisi tunasema kwamba mambo mazuri lazima yapigiwe upeto. Lile jumba liko sawa kabisa. Ile lift ambayo wanazungumzia ilikuwa inarekebishwa tu kidogo. Juzi nilienda kule na iko fresh kabisa . Mimi kama Mama Mombasa, nangoja niingie pale. Ofisi yangu hapa chini ilikuwa kama store . Kwa sasa, tuna ofisi nzuri sana. Kwa hivyo, wewe usichukuliwe vingine na wala usibabaike. Usisumbuliwe akili. Kaa hapo kama umekita na sisi tufanye kazi ili tujenge taifa pamoja. Ahsante sana, Mhe. Spika. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor"
}