GET /api/v0.1/hansard/entries/1415406/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1415406,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1415406/?format=api",
"text_counter": 151,
"type": "speech",
"speaker_name": "Matuga, ANC",
"speaker_title": "Hon. Kassim Tandaza",
"speaker": null,
"content": " Ahsante Bi Naibu wa Spika kwa kunipatia fursa hii ili niweze kuchangia katika huu Mswada muhimu. Kwanza nimpatie kongole Mhe Chepkong’a kwa kuuleta Mswada huu. Ukiangalia majukumu ya Seneti kama Katiba inavyosema, hakuna haja ya wakili kuweza kupambanua. Wao wanatakikana washugulikie masuala ya kaunti na jingine na endapo kutakuwa na mswada wa kuweza kumng’oa rais na naibu wake, hapo ndipo masuala kama hayo yanafika kwa Seneti. Lakini kwa hivi sasa, ni jambo la kuhuzunisha kwamba Seneti imeweza kuunda kamati sawia na zile za Bunge hili. Sisi tukiwa takriban 300 na zaidi hapa, wao wakiwa watu 60, wameunda kamati kama zetu. Utapata inabidi Seneta akae kwa kamati nne ama tano kwa sababu wenyewe ni wachache na kamati ni nyingi. Kama mwenzangu alivyotangulia kusema, ninapoangalia Kamati walizoziunda, inaonekana kwamba labda lengo ni kuwapatia fursa ya kusafiri nje au ndani ya nchi na labda kupata marupurupu kwa hizo mikutano. Najua wao wenyewe wanajua kwamba hawana ujuzi wala nguvu yeyote ya kutekeleza majukumu hayo."
}