GET /api/v0.1/hansard/entries/1415409/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1415409,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1415409/?format=api",
    "text_counter": 154,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Matuga, ANC",
    "speaker_title": "Hon. Kassim Tandaza",
    "speaker": null,
    "content": "Mswada huu utaweza kupeana mwelekeo na kuweka kinagaubaga kwamba hawakushurutishwa kwenda Seneti. Ikiwa wanataka majukumu zaidi, basi wanayo nafasi ya kuja Bunge ili waweze kushughulika na yale majukumu ambayo Bunge inahitajika kufanya. Lakini kwa sababu walienda Seneti kwa hiari yao, wajue kwamba wana majukumu yao ambayo pia si machache. Kama mwenzangu alivyotanguliza kusema, wao wenyewe wanayadharau. Labda wanaona hayana marupurupu ya kutosha. Matatizo ambayo yako kwa kaunti saa hii ni mengi sana. Ukiangalia masuala ya ukulima ambayo wanasema yamegatuliwa na ukulima ni uti wa mgongo wa uchumi ya Kenya, Seneti haijachukua hatua yoyote kuyatatua aidha kupitia kwa kamati ama kutengeneza sheria ambazo zitaweza kuhakikisha kwamba ukulima unafanyika, pembejeo zinapatikana na county governments wanapeana fedha za kutosha ili kusaidia wakulima. Katika zile kaunti waweze kuajiri watu wa kutosha ili kuhakikisha kwamba ukulima unafanyika na wakulima wanapata ushauri wakati unaofaa. Hawafanyi jukumu hili lao. Ajabu ni kwamba, endapo Serikali kuu ikijaribu kuwasaidia, inakua tena ni kero na kesi kwamba isifanyike. Kwa hivyo, jambo hili linafanya watu wasiweze kupata manufaa ya ugatuzi kama walivyokuwa wanatarajia. Jumba ambalo lingeweza kusawazisha mambo haya ni Jumba la Seneti. Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda. Naunga mkono Mswada huu."
}