GET /api/v0.1/hansard/entries/1415412/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1415412,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1415412/?format=api",
    "text_counter": 157,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Butere, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Tindi Mwale",
    "speaker": null,
    "content": "Jambo la kwanza, Bunge la Kenya lina vyumba viwili. Bunge la Taifa ambalo lina Wabunge Wateule na Bunge la Seneti. Mara kwa mara, tumeona shida nyingi sana kama kutoelewa ni nani anafaa kufanya kazi fulani. Kwa hivyo, namshukuru mwenzangu kwa kuleta Mswada huu ambao unaangalia mawasiliano katika vyumba hivi viwili, haswa kuhusu jambo la uangalizi ama kwa Kiingereza, oversight . Utapata Waziri anakuja katika Bunge la Taifa na kuzungumza kuhusu uangalizi wa fedha ambazo zimepotea. Pia unapata katika Bunge la Seneti huyo Waziri mmoja anaitwa na Kamati ya Seneti kujibu yale maswali ambayo aliulizwa katika Bunge la Taifa. Kwa hivyo, tukipata mwelekeo kupitia kwa huu mpangilio, kwamba maswali fulani yataulizwa na Kamati ya Bunge la Taifa na mengine yataulizwa na Kamati ya Bunge la Seneti, itakuwa bora Katika Bunge la 12, wakati wa kusoma Bajeti, tulikuwa tunakaa hapa sisi wote - Wabunge na Maseneta. Lakini kwa sababu ya kukosa mwelekeo, tulifika mahali Spika wa wakati huo, Mhe. Justin Muturi, akapeana mwelekeo kwamba Bajeti ikisomwa ni sisi pekee yetu tunafaa kukaa hapa. Kwa hivyo, huu Mswada unapeana mwelekeo, vile vyumba viwili vya Bunge la Kenya vitafanya kazi na kuweza kuwaridhisha Wakenya ndio wajue vile shida zao zinasuluhishwa. Ahsante."
}