GET /api/v0.1/hansard/entries/1416078/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1416078,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1416078/?format=api",
"text_counter": 445,
"type": "speech",
"speaker_name": "Taita Taveta County, UDA",
"speaker_title": "Hon. Haika Mizighi",
"speaker": null,
"content": " Asante, Mhe. Mwenyekiti wa Muda, kwa kunipatia hii fursa ili nichangie mabadiliko ya kurekebisha sheria za barabarani. Kabla sijaunga mkono—kwa sababu tunazungumzia mambo ya barabarani—ninatoa pole zangu kwa waliohusika katika ajali ya barabarani na basi la Chuo Kikuu cha Kenyatta kule Maungu, Voi, Kaunti ya Taita Taveta. Pia, ninatoa rambirambi zangu kwa familia zilizopatwa na msiba huo. Kama Mama wa Kaunti ya Taita Taveta, ninasema pole sana. Wakati sasa umefika wa kubadilisha hizi sheria za barabarani, ili kuwe na ufasaha. Ajali zimekuwa nyingi. Jumamosi, nitazika mwanafunzi aliyefariki baada ya kuhusika katika ajali ya barabarani kule Kapsabet. Misiba imekuwa mingi. Watu wanapoteza maisha kupitia ajali za barabarani. Ninaunga mkono mabadiliko haya. Ni wakati wa kuyafanyia kazi. Asante sana, Mhe. Mwenyekiti wa Muda."
}