GET /api/v0.1/hansard/entries/1418011/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1418011,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1418011/?format=api",
    "text_counter": 69,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Wundanyi, WDM",
    "speaker_title": "Hon. Danson Mwashako",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika. Nakushukuru kwa nafasi hii niweze kuwakaribisha vijana wa Chuo Kikuu cha Kenyatta kutoka Pwani. Hawa vijana, karibu mia moja kwa ujumla, waliona ni vyema leo watembee katika Bunge la Kitaifa ili wakaone ni vipi tunafanya kazi katika Nyumba hii ambayo imeheshimika. Hawa wanafunzi wamebobea sana katika masuala ya masomo tofauti tofauti. Kando na masomo, hawa ni viongozi ambao tunatarajia ndani ya miaka miwili, au mitatu, wanapomaliza masomo yao ya chuo, wengine wao watakuwa Wabunge, Maseneta na viongozi katika taifa letu la Kenya."
}