GET /api/v0.1/hansard/entries/1418169/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1418169,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1418169/?format=api",
"text_counter": 227,
"type": "speech",
"speaker_name": "Makueni County, WDM",
"speaker_title": "Hon. Rose Mumo",
"speaker": null,
"content": " Ahsante Bwana Spika wa muda kwa kunipatia nafasi ili nichangie Ripoti hii. Namshukuru sana Mwenyekiti ambaye ameleta Ripoti kuhusu watu wenye changamoto au kwa jina lingine tunasema, walio na ulemavu. Ripoti hii imekuja kwa wakati wake. Niseme kwamba sisi kama Wakenya hatulizingatii sana jambo hili. Njia ya kuwasaidia watu wenye ulemavu imekuwa ni shida kubwa. Tunapowangalia, wanaonekana kama hawawezi. Wale wachache ambao wamesoma na kupata umahiri wa kazi wanaweza kuandikwa. Ningeomba Kamati hii iangalie sana mambo ya watoto walemavu kuanzia pale shuleni. Unapata kwamba wale ambao wamesoma ni wale ambao wametoka katika familia zilizo na uwezo. Lakini ukiwa mlemavu na umetoka katika familia ambayo haina mapato vizuri, au kuna umaskini fulani, unakuta kwamba hata wewe kwenda shule ni shida. Hata kwenda katika shule ya upili inakuwa ni shida. Kwa hivyo, wanazidi kukaa nyumbani na kukosa kazi. Sheria zipo ambazo zimetungwa na ziko ambazo zinaelekeza kwamba watu wenye ulemavu waweze kusaidika na kuandikwa kazi. Lakini unapata kwamba hatuifuatilii ipasavyo. Ingekuwa vyema kuwe na sheria inayolazimisha kila ofisi ya Serikali au isiyo ya Serikali, kuajiri mtu mmoja mlemavu. Na ulemavu si kukosa kidole pekee yake. Utakuta kwamba wanasema wameajiri mtu mlemavu ilhali huyo mtu labda ana kidole kilichokatika. Tunataka waajiri watu walemavu kabisa. Tunataka pawepo watu wanaoweza kutembelea maofisi kuangalia kama sheria hii inafuatwa. Ninapoendelea kuunga mkono Ripoti hii, ningependa kusema kwamba zamani kulikuwa na social workers au wafanyikazi wa Serikali ambao walikuwa wanatembelea nyumba za watu kuangalia watoto wenye ulemavu. Lakini jambo hili limepungua na wazazi wengi unakuta hawawapeleki watoto wao shuleni kwa sababu ya kile wanachokiita kwa Kiingereza stigma, au kwa sababu wanahofia kwamba watoto wao wanaweza kuwa na laana fulani ambayo inasababisha ulemavu. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor"
}