HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1418565,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1418565/?format=api",
"text_counter": 253,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": "Kwa mfano, sisi kama Wabunge wa Pwani, tuli apply chakula cha kupatia walioathirika na njaa kutoka kwa Wizara ya East African Community, Arid and Semi-Arid Lands (ASALs),and Regional Development . Inatamautisha kuwa hata wale viongozi wa dini wameenda kutafuta msaada huo kwa kuwa ni haki yao, na wanawajua wanyonge katika jamii. Walivyokwenda katika Idara fulani kuuliza, wakaambiwa chakula kitapewa mtu fulani, ambaye ni mwanachama wa chama fulani ili akisambaze kaunti nzima. Rasilimali zetu zisifanyiwe siasa. Ndio maana ndugu yangu, Mhe. Owen Baya, amekuwa mkali kwa sababu mambo mengi yanafanywa kufinya watu wengine. Kama sisi sote tunafuata sheria ya Kenya katika mambo ya Idara ya Mikoa, basi tuhakikishe kuwa kila Mkenya anapata haki yake kulingana na Katiba. Haiwezekani chakula, kwa mfano, kimetoka kule katika Idara ya EastAfrican Community, Arid and Semi-Arid Lands (ASALs), and Regional Development, kikija Mombasa, Masheikh wanaambiwa hawawezi kukichukua, na kuwa kitachukuliwa na Mbunge fulani ambaye atakisambaza kaunti nzima. Chakula hicho sio cha kufanyia siasa. Leo napinga hapa vikali, nikisema Wabunge wenzangu tuangalie. Ukishachaguliwa katika kiti, usianze kufinya wananchi. Uko na vitu vingi unavyoweza kawafanyia wananchi, lakini mambo ambayo yanahusiana na taifa nzima na kila Mkenya, lazima uangalie kuwa yule mwenye idara amepewa mamlaka ya kuangalia kila mmoja bila kuangalia chama, kabila na rangi. Ndio maana sisi, kama Wapwani, tunasema tumefinyika sana. Watoto wetu wamesoma idara nyingi, lakini hatuwaoni kule sehemu zingine wala nyumbani. Ikiwa kama mgao wa idara tofauti unatokea katika mambo ya kikazi, sisi pia tuko na watoto wetu waliosoma. Kama watapelekwa kwa majani chai tuwaone wako kule, tutashukuru. Wale wakija kwetu, tutawapokea. Lakini sio kule kwao wanachukua kila kitu, na kwetu pia wanabakura kila kitu. Huo ndio uchungu ambao ndugu yangu, Mhe. Owen Baya, anasema. Tunasema wengi wape; usipowapa watajichukulia. Wakati utafika tutaanza kubisha kila mlango tuangalie takwimu zinaonyesha vipi. Ikiwa Mpwani katika idara fulani ambayo iko nyumbani ameachwa nyuma, basi itabidi nasi pia lazima tuingilie kati tuangalie tunarekebisha vipi. Licha ya hayo yote, huu Mswada ni mzuri sana; utaleta maendeleo mazuri, licha ya kuwa tunajua kaunti zinafanya kazi yao. Na hawa ambao ni wenye idara kutoka kila mikoa wana kazi zao, tunawapa nguvu. Isipokuwa wengine hujazana kwenye maofisi hujui wanafanya kazi gani, na tunasema uchumi uko vibaya. Hii mishahara za kudondoa kila mahali kupatia watu wengi ambao hatuoni kazi yao upunguzwe. Tupate mtu ambaye anaweza kufanya kazi kwa ustadi, anaeleweka vizuri, na ako na ueledi wa kufanya kazi, wafanye hata kama ni watu sita ama saba badala ya watu 11 kama ilivyokuwa zamani. Sisi tutashukuru sana. Kama Mama Mombasa, naunga Mswada huu mkono, ila urekebishwe uweze kugusa kila jamii ya taifa hili. Ugatuzi pia uheshimike na mamlaka haya. Watu waangalie kuwa wenye mji, mtaa na nchi wanapata vipi haki yao. Naunga mkono. Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda."
}