GET /api/v0.1/hansard/entries/1418852/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1418852,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1418852/?format=api",
"text_counter": 159,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bw. Spika wa muda, kwa ajili ya ulinzi, serikali ya Kenya Kwanza na Profesa, wanafanya kazi nzuri. Lakini, kwa wakati huu ambao mvua inanyesha sana, tungetaka amani. Tumeona viongozi wengi wakienda kusaidia watu kule vijijini. Kwa mfano, wale ambao walienda Mukuru kwa Njenga na kwa Reuben wakiambia watu wasitoke pahali wamejenga karibu na mto ilhali tunajua ya kwamba, wakijenga hapo, watasombwa na maji. Na kuuliza hili swali kwa sababu wewe ni mchapa kazi. Kwa ajili ya maslahi ya hao watu, mmechukuwa jukumu gani kwa wale watu ambao walichochea watu wasihame? Tunastahili kujua kama wamefungwa au wamepelekwa kortini ili jambo kama hilo lisifanyike tena. Na pia, tunajua kwamba walitamka matusi mabaya ya kusema kwamba watu wengine wanalala. Ukiwachukulia hatua kuanzia saa hii, itachukua muda kiasi gani ndio hawa watu wawekwe ndani ili tuwe na amani katika Serikali ya Kenya Kwanza. Asante."
}