GET /api/v0.1/hansard/entries/1418902/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1418902,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1418902/?format=api",
"text_counter": 209,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Thank you, Mr. Temporary Speaker, Sir. Mimi ninamshukuru sana Waziri wetu wa usalama kwa kazi anayofanya Kenya na pia hasa kwa kazi anayofanya Tana River. Makosa yalifanyika mara ya kwanza walipokuwa wanaweka ile kambi ya GSU, ni kuwa hawakuongea na jamii pale. Walienda wakatafuta mahali na watu wa usalama pekee yao na wakaweka. Hata hivyo, ninashukuru kwa sababu sasa amesema ya kwamba wameongea na wananchi. Ukweli ni kuwa Kulesa Village iko juu na wakiweka hapo kambi ya GSU, hatutapata hasara ya kuzama tena. Asante sana Bw. Waziri. Jambo ambalo umesahau ni kujibu sehemu ile ya swali kuhusu pengine ni lini ambapo unakisia tutaregesha ile kambi ya GSU. Hii ni kwa sababu sehemu ile haiko mbali sana na msitu wa Boni ambao uko na mushkil kila wakati. Kwa hivyo, ungetupatia huo muda tungeshukuru. Swali langu la pili na la mwisho ni kuhusiana na usalama wa sehemu hiyo. Tunashukuru sana Bw. Waziri alitupatia kaunti ndogo mpya, Tarasa. Waziri aligazeti hiyo kaunti ndogo, lakini hakugazeti makao makuu. Kweli kuna ushirikishaji wa umma uliofanyika na pengine ulipata maoni ya umma lakini baaadaye kulikuja maombi ya kugeuza hayo mazugumzo yaliyofanyika. Bw. Waziri, shida kubwa ni kuwa, kuna wasiwasi kwamba mvua ikiwa nyingi, mafuriko yataathiri sehemu iliyotajwa. Kwa hivyo, badala ya Serikali kuu kuingia hasara kama tulivyoingia hasara ya Kambi ya GSU, ingekuwa bora usifuate maneno yangu au ya viongozi wengine, lakini utume wataalamu wako mwenyewe, wakaangalie ni sehemu gani ingefaa ambayo hailoi maji. Huu ndio wakati mzuri kwa sababu mtu hawezi kukudanganya ununue shamba ambayo inaloa maji. Mtu hawezi kukudanyanga uweke"
}