GET /api/v0.1/hansard/entries/1418906/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1418906,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1418906/?format=api",
    "text_counter": 213,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "The Cabinet Secretary for Interior and National Administration",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "(Hon. (Prof.) Kithure Kindiki): Asante sana, Bw. Spika wa Muda. Ni kweli tulifanya makosa katika kuanzisha kambi yetu ya kikosi cha GSU katika sehemu ile ambayo baadaye tuligundua ni sehemu inayokumbwa na mafuriko. Kama Waziri, naomba msamaha kwa niaba ya wenzangu wote. Vilevile, tumerekebisha hayo makosa. Safari hii, kabla tuanzishe kambi mpya, lazima tuhusishe jamii kwa sababu wale maofisaa tunaotuma kwa kambi sio wetu, bali ni wa manufaa ya wananchi wa pale. Kwa hivyo, safari hii tumerekebisha makosa. Kama nilivyosema, naomba msamaha kwa sababu safari ya kwanza, hatukufanya mashauriano ya kutosha na umma na viongozi wa pale. Jambo la pili na la mwisho, Seneta wa Kaunti ya Tana River, Sen. Mungatana, amezungumzia suala la kaunti ndogo ya Tarasaa ambayo ilikuwa katika ile orodha ya kaunti ndogo kumi na sita ambazo tulizitangaza tarehe 10/2/2024 . Ilikuwa ya kwanza kwa sababu, kati ya zile kaunti ndogo tulizokuwa tunatangaza siku ile, ilikuwa the mostneedy case. Zote zilikuwa na uhitaji mkuu, lakini hiyo was a special case. That is whywe started with Tarasaa. Ni kweli hatukutangaza makao makuu ya kaunti ndogo na ilikuwa maksudi kwa sababu wakati tunapotangaza eneo la Serikali na kuweka katika gazeti rasmi ya Serkali, tunatangaza makao makuu kama jamii ya pale imeshakubaliana, through a participatoryprocess and there is no difference of opinion . At least a majority of the people have agreed and there is evidence because, ukishaweka katika gazeti rasmi la Serkali, inakuwa sheria. Pili, hungetaka Serikali iwe inaingiliana na wananchi wakati wanaamua mambo yao. Ungetaka uwaache wananchi waamue, na pindi watakapopata maamuzi ya walio wengi, Serikali inakuja kutekeleza matakwa ya wananchi. Hiyo ndio maana ya publicparticipation. Kwa hivyo, tumekubaliana ya kwamba tutaondoa kambi mpya ya GSU mahali ilipo, tuiweke mahali palipo juu. Tutafanya hivyo chini ya siku thelathini kutoka leo. Vile vile, kwa sababu lile ni eneo hatari ambalo liko pembeni mwa msitu wa Boni, tutafanya hivyo. Nimeshatoa amri kwa maafisa wangu wakuu hapa. I have some seniorofficers here. Tutatuma wataalam wasioegemea upande wowote kuangalia hali ilivyo sasa kwa sbabau maji yako sehemu ya chini. Hiyo team itatumwa kufikia Ijumaa na tunatarajia wapewe wiki moja ili walete ripoti. Hio ripoti ikifika tutawajulisha viongozi halafu tutaweka kambi kwa muda wa siku 30. Ni hayo tu kwa sasa, nashukuru Bw. Spika wa Muda."
}