GET /api/v0.1/hansard/entries/1418936/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1418936,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1418936/?format=api",
    "text_counter": 243,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Asante sana Bw. Spika wa Muda kunipa fursa hii. Kwanza namshukuru Waziri wa Usalama kwa kazi nzuri anayotenda. Sio kwa mambo ya mafuriko na usalama peke yake. Swali langu ni hili. Kuna hii Independent Policing Oversight Authority (IPOA). Sijui mnafanya kazi nayo namna gani. Nikitembea Kaunti ya Laikipia, maafisa wengi wa usalama nasikia hawana motisha. Hii ni kwa sababu, juzi mahali panaitwa Kariunga askari wa National Police Reservists (NPR) alipigwa risasi na kuawa. Mahali panaitwa Mutara, mzee wa Kanisa anaitwa Muriuki alipigwa risasi na kuawa. Hapo karibu kuna pia askari polisi wa Anti Stock Theft Unit (ASTU). Lakini, askari wanapofika na wanaona majambazi, badala ya kuwapiga risasi moja kwa moja, wanafyatua risasi hewani kwa sababu wanaogopa wakiitwa na IPOA. Wao na familia zao watakuwa katika shida. Sijui Waziri mnafanya kazi kwa njia gani na IPOA kwa sababu inavunja moyo askari wetu wa usalama. Nimekuwa nikiongea na wao, wanaogopa. Wananiambia, Seneta, mimi nikipiga mwizi risasi, nitaulizwa maswali. Sasa nashindwa kama IPOA ndio watakuwa wakitulinda ama polisi? Asante."
}