GET /api/v0.1/hansard/entries/1419046/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1419046,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1419046/?format=api",
"text_counter": 98,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Ningependa kuwasihi madaktari pamoja na wauuguzi na wahusika wote, wakubali kurudi katika meza wakubaliane. Tunaelewa kuwa wana yale matakwa ambayo wangetaka yazingatiwe. Lakini kulingana na vile ambavyo yale matakwa ya kwanza waliyoyaongea kama wale interns, walisema wangetaka wote kuajiriwa na vile vile kulipwa takriban shilingi elfu sabini na hayo yalikubalika. Kulingana na vile ambavyo nimesikia ripoti tuliyopewa, ni vizuri wale madaktari na wauuguzi wakubali ya kwamba hakuna mtu yeyote amekataa kusikiliza matakwa yao, lakini kwa wakati huu, kwa vile ambavyo hakuna hela; hela ambazo zimepatika tayari serikali imekubali na vile vile wamekubaliana na wale ambao wanawakilisha madaktari haya mambo yatawezekana. Lakini mgomo huu umeendelea na ukitembelea hospitali zetu, utaona kwamba wananchi wanasononeka na wanapata shida. Mimi ninaomba waketi na waweze kukubaliana kwa sababu fahali wawili wapiganapo, nyasi ndizo huumia. Wanaoumia ni wananchi wa Kenya. Watu wawache kuwa na misimamo migumu. Nimewaona madaktari wakiwa na msimamo mgumu, hawaendi mahali ambapo wanaitwa ili kujadili mambo haya nao magavana wanafanya mikitano na hawawezi kuwaita. Vile vile, kuna mambo muhimu ambayo yameulizwa na hawa madaktari wa mahabara, walikuwa wanaomba waangaliwe na wanapofikisha kiwango fulani wanapaswa kukubalika katika kaunti zetu wajiandikishe kama kikundi. Magavana wetu wametupilia hilo wazo; hawajaliangalia. Kila mtu anapaswa kusikilizwa kwa sababu tukiendelea na misimamo hii ambayo ni mikali wale watakaoumia ni wananchi wa Kenya. Ninawasihi madaktari kwamba mambo wanayoyasema tumeyakubali na tunayaelewa, lakini waweze kupatiana muda. Wamekuwa wakisema haya maneno lakini ninajua machahe waliyoyasema yamesikizwa. Sasa wao wakubali kurudi kazini ili waweze kuhudumia Wakenya kwa sababu ni dada zao, ndugu zao, wazazi wao na sisi wote tunataka nchi yetu iendelee mbele. Asante."
}