GET /api/v0.1/hansard/entries/1419076/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1419076,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1419076/?format=api",
    "text_counter": 128,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii kutoa kauli yangu juu ya ripoti ya Kamati ya Afya iliyowasilishwa na Sen. Mandago, Seneta wa Gatuzi ya Uasin Gishu. Mgomo wa madaktari umekuwa donda sugu kwa sababu umeendelea zaidi ya mwezi mmoja sasa na hakujakuwa na muafaka wa kuutatua. Tukiangalia sehemu nyingi, wananchi wanapata shida, hususan wakati huu ambapo kumeingia mafuriko na mkurupuko wa magojwa kadhaa yanayosababishwa na maji. Ipo haja ya Serikali kukubaliana na madaktari kwa sababu wanawatumikia wananchi wa Kenya na pesa zinazolipwa wao ni za Wakenya. Sioni sababu gani Serikali ikae ngumu wakati wale wanaotaka kusaidiwa ni madaktari wanaofanya kazi muhimu katika nchi yetu. Binafsi nilitembelea hospitali kuu ya mkoa wa Pwani tarehe 1/5/2024 na nikaona kwamba, huduma nyingi zilikuwa zimesitishwa isipokuwa zile muhimu tu au za dhahura. Kwa mfano kama wodi ya watoto ambayo ilikuwa inafanya kazi. Watoto wengi walikuwa wanahudumiwa wakiwa wamelazwa kwa sababu ya magonjwa tofauti. Jambo la kufurahisha ni kuwa madaktari waliokuwa wanahudumia watoto wale walikuwa wamejitolea licha ya kwamba walikuwa na hisia za kushiriki na wenzao katika mgomo ili kuhakikisha kuwa matakwa yao yamepatikana."
}