GET /api/v0.1/hansard/entries/1419078/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1419078,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1419078/?format=api",
    "text_counter": 130,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Bw. Spika, masuala ambayo yanazungumziwa na madaktari ni ya kimsingi. Haya ni masuala ambayo mfanyakazi yeyote ni lazima awe nayo ili aweze kufanya kazi kwa utulivu akijua kuwa haki zake zimelindwa. Mwaka juzi tulipokuwa na janga la COVID- 19, madaktari wengi pamoja na wauguzi walipoteza maisha yao kwa sababu ya kukosa kinga. Mambo ambayo madaktari wanapigania ni mambo ya kimsingi kama ukosefu wa bima ya afya na mishahara ambayo iko chini ya kiwango wanachostahili kulipwa. Seneta Cherarkey alizungumza kuwa madaktari wanalipwa vizuri kuliko wakili ambao hawajahitimu. Ni kweli kwa sababu walinegotiate na Serikali na wakakubaliana kulipwa pesa hizo. Serikali haiwezi kuja baada ya miaka mitatu na kusema kuwa pesa wanazolipwa ni nyingi kwa hivyo zipunguzwe. Tumeona bajeti ya Serikali imeongezeka maradufu. Tumeone juzi bajeti ya Cabinet Administrative Secretary (CAS) na wengine wanaohusika. Kwa hivyo, hili ni suala la ubadhirifu wa rasilmali. Huu ni mwaka wa pili kutoka Serikali hii ya Kenya Kwanza iingie mamlakani. Waliweza kulipa kile kiwango kwa miaka hivi miwili. Ni jambo gani limefanya wasilipe mwaka huu na kurudi nyuma kuhusiana na mwafaka uliopatikana miaka saba iliyopita? Bw. Spika ni lazima Serikali irudi nyuma ikubaliane na matakwa ya madaktari kwa sababu wanayoyataka mengine tayari yako. Sio mambo mapya yanatakikana kufanyika."
}