GET /api/v0.1/hansard/entries/1419185/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1419185,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1419185/?format=api",
"text_counter": 237,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Khalwale",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 170,
"legal_name": "Bonny Khalwale",
"slug": "bonny-khalwale"
},
"content": "Asante Bw. Spika wa Muda. Wiki iliyopita nilikuwa nachangia Hoja hii, lakini kwa bahati mbaya nikapitwa na wakati. Ningependa kuendelea na mchango wangu na kukumbusha ndugu zetu kutoka Pwani kwamba sisi tunawaunga mkono kwenye Hoja hii muhimu, pia kwenye kuimarisha sera ya kandanda nchini. Watu wa Pwani wamechangia kwenye umaarufu wa soka nchini. Nilikuwa napitia orodha ya majina ya wale ambao walifana sana katika uchezaji wa mpira. Nimepata kwamba kwa wale 50 bora nchini, sita wametoka Pwani. Wameongozwa na aliyekuwa mchezaji wa AFC Leopards, Mohamed Abass. Pia tulikuwa na kipa wa kimataifa Bw. Mohamed Magogo aliyekuwa wa Pwani. Bw. Amram Shimba alikuwa mchezaji Hodari. Vile vile Badi Ali, Ahmed Breik na Ali Sungura. Bw. Spika wa Muda, kwa sababu ya mchango wa wachezaji hawa kwenye kandanda nchini, ni lazima uwanja huu wa michezo ujengwe na ukamilike ili iwe moja ya kumbukumbu. Tunatarajia kwamba ndani ya uwanja huu wataweka hall of fame ambapo majina ya wachezaji niliotaja itaweza kuandikwa. Wachezaji hawa walicheza na wachezaji wengine kutoka kwangu. Babu ya bibi yangu, Elijah Lidonde, alikuwa mmoja wa wale walioshinda Gossage Cup, mwaka wa 1962, mashindano ambayo ilichezewa Mombasa. Elijah Lidonde alikuwa na sifa kiasi ya kwamba, kabla astaafu alikuwa amefunga mabao 32 ya kitaifa. Naunga hii Hoja mkono kwa sababu hii ni njia rasmi ambayo tunaweza tumia kutafutia watoto wetu kule Pwani ajira. Wakati huu vijana wanaocheza kandanda wanalipwa mshahara wa juu kuliko wataalamu wengine wote. Ukilinganisha na mchezaji bora anayeitwa Erling Haaland anayechezea Manchester City--- Huyo kijana analipwa Kshs300 milioni kila mwezi. Talanta kama hii ambayo iko na watoto wetu kule Pwani tunataka tuikuze ili wapate ajira. Hii itakuwa njia mwafaka ya kupigana na ufisadi. Bw. Spika wa Muda, ingawaje ndugu yetu, Sen. Faki, anatuomba tumuunge mkono kwa kuuliza Serikali kuu ijenge uwanja huu wa kitaifa, tusisahau kuwa kupitia pesa za National-Government Constituencies Development Fund (NG-CDF) waheshimiwa wawili katika taifa hili walianzisha ujenzi wa stadia. Wa kwanza alikuwa Mhe. John Michuki aliyetumia CDF kuanzisha ujenzi wa uwanja na wapili na wa mwisho ni mimi, Sen. (Dr.) Khalwale, ambaye nilianzisha ujenzi wa Malinya Stadium. Kwa hivyo, Members of Parliament wako na nafasi kubwa ya kuchangia maneno ya spoti. Serikali ya Kaunti ya Mombasa, kwa sababu ya umuhimu wa spoti kwenye maisha ya watu wa Pwani, sioni kinacho zuia Gavana wa Mombasa kuendelea na ujenzi wa Mombasa Stadium, ambayo aliyekuwa Gavana Mhe. Joho alikuwa amefikiria kuijenga."
}