GET /api/v0.1/hansard/entries/1419189/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1419189,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1419189/?format=api",
    "text_counter": 241,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Oketch Gicheru",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Bw. Spika wa Muda, nimesimama kwa kufuata Kanuni zetu za Kudumu 101 kuhusu Maudhui ya Hotuba. Sipendi kumsimamisha Seneta wa Kakamega anapoongea kwa sababu mimi huwa napenda maarifa yake kwenye Hoja kama hii. Lakini je, ni vyema kumuongelea mtu ambaye hayuko kwenye Jumba hili kama Mhe. Joho, aliyekuwa Gavana wa Mombasa, akijaribu kuangalia na kuashiria mambo ambayo Gavana Joho alifanya, ambayo sisi kama Bunge hatuna ushahidi wowote? Angewachana na Gavana Joho na kuzungumzia uwanja tunaojadili. Ikiwa anataka kumzungumzia Gavana Joho, alete Hoja Bungeni, na tutaongelea hoja ile kwa undani."
}