GET /api/v0.1/hansard/entries/1419196/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1419196,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1419196/?format=api",
    "text_counter": 248,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Khalwale",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 170,
        "legal_name": "Bonny Khalwale",
        "slug": "bonny-khalwale"
    },
    "content": "Bw. Spika wa Muda, ningeomba ndugu yangu, Sen. Oketch Gicheru, akumbuke Kanuni za Seneti hii kuwa kabla ripoti ya Muhasibu Mkuu iletwe kwa kamati huwa inawasilishwa hapa. It is tabled halafu ndio inaenda. Hati yoyote ikishawakilishwa hapa inamaanisha sasa iko katika rekodi ya hii Seneti. Kwa hivyo, kila Seneta ako huru kuzungumzia mambo ambayo iko katika hiyo ripoti. Hii ndio maana nilikuwa nasema tena kwa heshima kwamba ndugu yangu Gavana wa sasa, Abdulswamad, ikiwa ataanzisha ujenzi huu, atakuwa amemufunika uchi ndugu yetu Mhe. Joho. Hii ni kwa sababu, hundi ya Kshs500 milioni aliyotumia kwa huo uwanja wa michezo haijulikani mahali ilienda."
}