GET /api/v0.1/hansard/entries/1419200/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1419200,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1419200/?format=api",
    "text_counter": 252,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Beth Syengo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii kuchangia Hoja ambayo imeletwa na Seneta wa Mombasa kuhusu ujenzi wa uwanja wa kimataifa wa michezo kule Pwani, Mombasa. Hakika wana Pwani ni wapenda michezo, riadha, mipira na wanahusika sana kwa mambo ya michezo ambayo inapendeza. Tunajua kwamba wana Pwani wanapenda starehe na kwa hivyo ni vyema kupata uwanja wa michezo ambao utawapa hiyo nafasi ya kufurahia, kushangilia, kuhudhuria na kuhusika ndiposa hata wao wausike kwa ujenzi wa taifa. Tunajua kwamba wakiwa na talanta za michezo kama mipira ama aina zozote zile za michezo, itakuwa inawapa mapato ya kila siku. Wanaweza kupata fedha na watajijenga kibinafsi kama jamii na itakuwa ya maana sana. Bw. Spika wa Muda, Kenya inatarajiwa mwaka huu kuandaa michezo ya East Africa Legislative Assembly (EALA) games ya wabunge wa Afrika Mashariki. Kwa hivyo, hizo bunge zote zikija pamoja kutoka nchi tofauti tofauti, tunahitaji uwanja kama huo unaopendekezwa hapa. Kwa kweli, tumependekeza kwamba michezo kama hii ifanyike kule Pwani. Huo uwanja ungekuwepo basi ungekuwa ya maana sana. Badala ya kutoa wachezaji kutoka Mombasa na wengine wakacheze kule Kwale, Nyeri ama kaunti tofauti tofauti, yote yangefanyika katika kaunti ya Mombasa. Kwa hakika itakuwa njia moja ya kuajiri vijana wetu na wanarika kwa kukuza talanta zao na wajitokeze kwa wingi kupata mapato ya maisha yao. Uwanja kama huu ni muhimu hata ninaona kama umechelewa. Ungefanyika mapema. Kama Serikali Kuu imefadhili viwanja kama hivi kwingine, kwa nini isifanyike Pwani? Tukiangalia kwa orodha ya kaunti vile Mungu alitumia waliohusika kuandika na kuleta Katiba mpya ama katiba iliyoko saa hii, Mombasa inaitwa Kaunti 001, kwa hiyo tunaanzia huko. Hata mambo ya michezo ianze kutoka Pwani ikienda kule kwingine. Ninamuheshimu sana Seneta wa Kakamega, Sen. (Dr.) Khalwale, na ni rafiki yangu wa karibu. Kama vile, amesema hakika kuna wale wanatalanta kutoka kule Pwani. Tumeona wameletea nchi yetu ya Kenya sifa mara dufu. Kwa hivyo, ni vizuri wawe na uwanja kama huu. Ni vyema wajivunie kwamba waliotangulia kuwa wachezaji kuletea sifa katika nchi ya Kenya, pia wanakotoka kumekuwa na uwanja wa kimataifa. Wako na nafasi ya watoto wao ile talanta ipitie kutoka kwa wazazi, iende kwa watoto hata kwa vitukuu. Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa sababu hili ni jambo la muhimu. Niongeomba pande zote mbile, pande ya Serikali na Upinzani, sisi wote tuunge mkono hii Hoja iliyoletwa na Seneta wa Mombasa, Sen. Faki, ili tujenge Kenya pamoja."
}