GET /api/v0.1/hansard/entries/1419204/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1419204,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1419204/?format=api",
"text_counter": 256,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "lazima pia tungecheza boli. Ni kama ni kawaida yetu mkiwa watoto watu wanaenda ufukoni, wanaongelea na kucheza boli na hiyo ni kitu kinayochofanywa kila siku. Kwa hivyo, ile tamaduni ya kucheza mpira uko sana sehemu za Pwani. Sisi tukiona kwamba sehemu zingine kunajengwa nyuga kubwa kubwa za kimataifa, lakini sehemu yetu ya Pwani haijajengwa uga kama huo, hatusikii vizuri. Mimi naunga mkono hii Hoja. Pia ninakumbuka nilipochaguliwa mara ya kwanza kama Seneta, kulikuwa na ratiba ya Serikali Kuu ambapo Waziri alisema wana haja ya kujenga viwanja vya kimataifa katika Kenya. Mimi nilienda kuomba mahali ambapo Serikali Kuu waweza kuweka hela ama raslimali ili kujengwe uwanja wa kutosha katika Tana River. Kati ya vitu ambavyo vilikuwa vinatakinana ni mahali pa kujengwa. Nilifuatilia kwa Wizara na walisema kabisa kwamba Munispaa ya Mombasa, ule uwanja ni mdogo na nafasi ni ndogo ilhali wanataka kujenga mahali pakubwa. Mimi niliweza kuwaambia kwamba Tana River kuna nafasi kubwa. Kaunti yetu ni kubwa na ina nafasi ya kutosha ya kujenga uwanja mkubwa wa kimataifa. Uwanja ambao utatumika, sio kwa michezo tu lakini pia kwa mambo ya training na mambo kama hayo. Watu hufikiria kwamba Tana River ni mbali lakini ukitoka Malindi na utembee tu kwa saa moja unafika Garsen hapo karibu na uto wa bahari. Lakini waliniambia uwanja wa Mombasa uko na shida ingine. Kwamba kuna mradi ambao ulianzishwa pale, pesa zilitumika vibaya. Wasimamizi wa huo mpango waliharibu kwa kufuja pesa za wananchi. Kwa hiyo, wao kama Serikali Kuu hawawezi kuingilia mpaka maswali yajibiwe. Kwa hivyo, mimi ningesema kwamba sisi kama watu wa Pwani ni kweli tunataka uwanja wa kimataifa wa kisasa ujengwe, lakini tuseme ati sasa pesa zilizowekwa pale zimepotea na hazijulikani ziko wapi. Halafu tena tuseme Serikali Kuu ije iweke hapo. Naona kama hapo hatutaelewana. Kwanza, wale waliohusika wakamatwe ili tujue pesa zile zilienda wapi, halafu baada ya hapo, Serikali kuu inaweza kuingilia kati. Lakini mambo ya kufichiana si mazuri. Ikiwa magavana wengine wa serikali zilizopita wanafuatwa hata wakishamaliza muhula wao, kwa nini wengine wasifutwe? Kama kuna pesa ziliingizwa pale na zimepotea, kwa nini tusiulize maswali? Tunataka ukweli ujulikane kabla ya pesa zengine kuwekwa pale. Namshukuru Gavana Abdulswamad kwa sababu hajaweka pesa pale mpaka maswali yajibiwe ili tujue ukweli ukoje. Tujue zile pesa zilizowekwa pale mwanzo ziko wapi, halafu tuendelee na kujenga. Na sio lazima ijengwe pale Mombasa Town kwa sababu hakuna nafasi ya kutosha. Watu wanaweza kuenda nje kama Mtwapa kuelekea Kilifi ambapo mashamba yako ya kutosha na nafasi iko. Watu wajenge uwanja wa kisasa. Lakini kufichiana kwa kusema Serikali kuu ije iweke pesa, hizi pesa ni zetu. Haiwezi kuwa tunatumia tu ilhali wengine wanajificha na wamepata utajiri ambao haueleweki. Bw. Spika wa Muda, Hoja hii igeuzwe kidogo. Ni kweli tunakubaliana kwamba tunataka uwanja, lakini isiwe kwamba tunafichiana. Kwanza ukweli ujulikane ndio Serikali kuu iingilie. Kwa hayo machache, Asante Bw. Spika wa Muda."
}