GET /api/v0.1/hansard/entries/1419207/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1419207,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1419207/?format=api",
    "text_counter": 259,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Omogeni",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13219,
        "legal_name": "Erick Okong'o Mogeni",
        "slug": "erick-okongo-mogeni"
    },
    "content": "Bw. Spika wa Muda, pia mimi naomba nizungumze kwa lugha ya taifa. Nasimama kuunga Hoja hii iliyoletwa na rafiki yangu, Seneta wa Mombasa, Sen. Faki. Wakati tulipokuwa tunaangalia mpira wakati nikiwa mdogo, siku zile ambazo timu yetu ya Harambee stars ilikuwa inawika sana, tulikuwa tunamheshimu goalkeepe r mmoja aliyeitwa Mohamed Abass. Yeye alianza kucheza mpita akiwa kule Mombasa, akichezea timu iliyokuwa inaitwa Feisal Football Club kule Mombasa, na akaja akajiunga na Club ya AFC Leopards, na akawa goalkeeer maarufu sana katika kanda ya Afrika Mashariki na hata Kati. Wakati huo huo kulikuwa na mashindano yanayohusisha nchi za Afrika Mashariki na Kati. Kwa hivyo, watu wa Mombasa wanapenda sana mpira sana. Ikiwa Seneta wao, ambaye ni mchezaji shupavu sana, ambaye huwa anachezea timu ya Bunge la Kitaifa katika michezo ya Mabunge ya Afrika Mashariki, ameleta Hoja hii kuomba kwamba apewe Kshs1.7 bilioni ili Kaunti ya Mombasa ijenge uwanja wa mpira, namuunga mkono. Bw. Spika wa Muda, unavyojua michezo katika nchi za ulaya ni kati ya industries ambazo zimepatia umaarufu vijana wengi na wameweza kujisimamia kupata hali nzuri ya maisha kupitia michezo.Kwa hivyo, naomba Maseneta wote waunge mkono Hoja hii iliyoletwa na Mhe. Faki. Kenya tumewasilisha maombi ya kufanya ile michezo ya Africa Cup of Nations (AFCON). Kama tunataka kushinda katika ombi letu la kuwa na hiyo michezo katika nchi yetu, sharti tuwe na viwanja vilivyo katika hali ya kimataifa. Miji yetu mikuu kama Kisumu, Nakuru, Mombasa na Kakamega inahitaji viwanja vilivyoko katika viwango vinachokubaliwa kimataifa na lile shinikizo la kandanda la Federation Internatinale de Footbal Association (FIFA). Kwa hiyo, naunga Hoja hii ya Mhe. Faki. Mwaka huu tutakuwa na bahati sana Mungu akitujalia kuwa waandalizi wa michezo ya Mabunge Afrika Mashariki na Mombasa ndio mji utakao host michezo hiyo. Tutakuwa tumepeleka ujumbe mzuri kwa watu wa Pwani sisi kama Wabunge tukienda kule kwa hii michezo. Pia tuwapatie zawadi kuonyesha kama Serikali kuu, tumewapatia pesa ya kujenga uwanja wa kimataifa wa mpira kule kaunti ya Mombasa. Maneno ya kujenga viwanja hivi sio rahisi. Katika kaunti ya Nyamira, tumejaribu kuujenga uwanja kwa miaka 12 sasa na bado hatuna uwanja. Kila wakati tunapomwalika Gavana wetu aje, yeye husema tungoje miezi sita ili uwanja ujengwe. Hadi sasa hivi hatuna uwanja. Hapo awali tulikuwa na wakimbiaji kutoka kaunti yetu ambao walishinda medali ya dhahabu katika michezo ya miaka 1972 kule Munich, Berlin, Nyandika Maiyoro. Kwa hivyo, sisi ni watu wanaopenda michezo sana. Ukitazama michezo ya kukimbia mita 800, anayevunja rekodi sasa ni mtoto wetu kutoka jamii ya Omogusii, Hellen Obiri. Akiingia uwanjani kukimbia mbio za mita 10,000 ama katika"
}