GET /api/v0.1/hansard/entries/1419217/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1419217,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1419217/?format=api",
"text_counter": 269,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Cherarkey",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13217,
"legal_name": "Cherarkey K Samson",
"slug": "cherarkey-k-samson"
},
"content": "Bw. Spika wa Muda, kulingana na Kanuni ya Kudumu ya Seneti 105 lazima Seneta awe na uhakika na yale ambayo anasema na yanayonakiliwa katika rekodi ya Taarifa rasmi ya Seneti. Je, ni kweli kwa kiongozi, Wakili, Sen. Omogeni, kuonyesha dhana ya kwamba mimi mstahiki na mwenye heshima zangu kama kiongozi, nadhalilisha ama nakosa heshima kwa madaktari? Hiyo ni haki kweli ilhali mimi najulikana kumheshimu kila mtu hata yule hajazaliwa? Naomba aondoe na aombe msamaha mara moja."
}