GET /api/v0.1/hansard/entries/1419231/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1419231,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1419231/?format=api",
"text_counter": 283,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Oketch Gicheru",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "mikaka. Mimi kama kijana anayetoka jamii inayopenda michezo, sikujua kwamba ukienda Pwani hautapata viwanja kule. Vijana wanaweza enda kucheza na pia wafunzwe maneno mazuri ili wajikinge na lile janga la kukaa tu bila michezo au kuhusishwa na mambo ya michezo kila saa. Ni muhimu sana vile Seneta wa Mombasa ameonelea ni vyema Jiji la Mombasa liwe na uwanja kama huu. Sisi kama Seneti tunafaa kuunga hii Hoja mkono ili uwanja ujengwe pale. Jambo la tatu, ukiangalia historia ya Kenya, kuna jamaa anayeitwa Dennis Oliech. Huyu kijana ni wa pili Kenya hii, nyuma ya kijana anayeitwa Ouma William Chege kwa kuweka mabao katika michezo ya kimataifa. Ouma William Chege alifunga mabao 35 na Dennis Oliech alifunga mabao 34 wakati walikua wanachezea timu ya Harambee Stars. Bw. Naibu wa Spika, huyo Dennis Oliech mwaka wa 2004, alisimama na nchi yetu wakati tulikuwa tunajaribu kuingia michezo ya African Cup of Nations (AFCON). Yeye ndiye alifunga lile bao lililotupeleka pale ili tucheze mpira kwa hiyo michezo. Wakati tulipokua tunashiriki mashindano hayo kule Burkina Faso, tulifunga timu ya Burkina Faso mabao matatu kwa nunge na Dennis Oliech ndiye alikua wa kwanza kufunga hayo mabao. Mpaka leo Dennis Oliech hajawahipatiwa ile heshima yake katika nchi yetu. Ukiangalia kule Mombasa na Pwani yote, kuna vijana wanacheza mpira wa hali ya juu sana, lakini ndoto zao za kwenda mbali au kuchezea vilabu vikubwa nje ya nchi au bara la Africa haziwezi timika kwa sababu hawapati vifaa vya kisasa ili wajiendeleze kimchezo na wasimamie jamii zao. Sisi kama jamii ya Kenya, tunajua wachezaji kama wanariadha, wanasoka na wa michezo ingine iliyo nchi yetu ni watu wanaoletea nchi yetu sifa kubwa sana. Itakuwa juhudi yetu kama Seneti ili kusaidia Sen. Faki apate hizi pesa na apelekee Ustadh mwenyewe, Sultan wetu pale, Gavana Abdulswamad Nassir, ili atengeneze huu uwanja ili vijana wa Mombasa wapate nafasi ya kucheza soka vilivyo. Bw. Spika wa Muda, nimeona pia Serikali ya Kitaifa imejaribu kutengenezea vijana kazi. Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki watakakuja huku kushiriki michezo ya kila mwaka. Kwa hivyo, ni vyema watu wa Mombasa wapewe pesa kwa haraka ili Uwanja wa Michezo wa Manispaa ya Mombasa utengenezwe ili vijana wa Pwani wapate kazi."
}