GET /api/v0.1/hansard/entries/1419251/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1419251,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1419251/?format=api",
"text_counter": 303,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Oketch Gicheru",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Sasa Bw. Spika wa Muda, alijaribu kunikosoa na nikasema ya kwamba ningependa kumsaidia kwa sabubu haelewi mambo ya mpira. Nimesema ya kwamba kabla mchezaji Ouma Chege astaafu alifungia timu yake ya Harambee Stars ambayo ni timu ya Taifa, mabao mengi. Hatuwezi ongea kuhusu Olunga kwa sababu hajastaafu kucheza mpira. Bado anacheza mpira. Ouma Chege alistaafu akiwa amefungia Harambee Stars mabao 35. Oliech alifungia Harambee Stars mabao 34. Ndiposa nilikuwa nasema kabla ya kustaafu. Na unajua kwa sababu yeye ni daktari ambaye hakustaafu kabla kuingia kwa siasa, hajui maana ya kustaafu. Sasa nitamwambia maana ya kustaafu nje ya Bunge. Namalizia kwa kusema, ingekuwa vizuri kwa sababu Katiba, katika Kipengele cha 203 inapatia Serikali ya Kitaifa mamlaka ya kupatia kaunti pesa za ziada wakati wowote ingetaka kufanya hivyo."
}