GET /api/v0.1/hansard/entries/1419253/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1419253,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1419253/?format=api",
"text_counter": 305,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Oketch Gicheru",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Mwezi huu tunatengeneza bajeti. Ningeomba kwa niaba ya watu wa Pwani na ndugu yangu Sen. Faki, Serikali iende kwa haraka iwape hii pesa ili waanze kutengeneza hivi viwanja mwezi wa saba au wa nane. Wakati Jumuiya ya Wabunge ya Africa Mashariki watakuja Mwezi wa 12, ingekuwa bora zaidi tuwe na ule uwanja pale Mombasa ili watu wajumuike. Hata wewe Bw. Spika wa Muda Wakili Sigei, juma lililopita nilikuwa kwako. Nilipata umeandaa mchezo mkubwa pale. Uliona vile uwanja ulikuwa umefurika pale Bomet. Vijana, wamama, wazee na jamii yote walikuwa wamekuja kucheza mpira pale Bomet. Hata mimi, nilikuwa niko na furaha zaidi kwa sababu jamii yote ilikuwa imejumuishwa katika mchezo. Ni vyema watu wa Pwani wangekuwa na ile cheche na mbwembwe, haha na hoihoi wakati watakapo pata uwanja mzuri ulio na vifaa vya kisasa wacheze mpira na wajumuike na Wakenya kufurahia kuwa na uwanja mzuri. Kwa hivyo, naiunga hii Hoja ya ndugu yangu Sen. Faki. Ningependa kusema kama kijana barubaru ambaye yuko katika Seneti---"
}